Mwenyekiti wa Wanawake Wizara ya
Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Prisca Shewale akikabidhi vitu
mbalimbali kwa niaba ya wanawake wa Wizara hiyo kwa Mganga Mfawidhi wa
Kituo cha Afya Chamwino Dkt.Zipora Mfugale kwa ajili ya wanawake,
watoto na wenye uhitaji maalum waliolazwa kituoni hapo ikiwa ni
kuamdhimisha Siku ya Wanawake Duniani leo Wilayani Chamwino.
Afisa Utumishi Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Jacquiline Kalua akimpa vifaa
mbalimbali Bibi Marietha Maiko alielazwa Kituo Cha Afya Chamwino wakati
wanawake wa Wizara hiyo walipotembelea kituo hicho katika kuamdhimisha
Siku ya Wanawake Duniani leo Wilayani Chamwino.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Lorietha
Laurence akitoa vifaa mbalimbali kwa Bibi Regina Balabaido alielazwa
Kituo Cha Afya Chamwino wakati wanawake wa Wizara hiyo walipotembelea
kituo hicho katika kuamdhimisha Siku ya Wanawake Duniani leo Wilayani
Chamwino.
Afisa Habari wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi.Lilian Lundo akitoa vifaa
mbalimbali kwa Bibi Molen Mwaiko alielazwa Kituo Cha Afya Chamwino
wakati wanawake wa Wizara hiyo walipotembelea kituo hicho katika
kuamdhimisha Siku ya Wanawake Duniani leo Wilayani Chamwino.
Baadhi ya Wanawake Wizara ya
Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na
uongozi wa Kituo Cha Afya Chamwino mara baada ya kutembelea Kituo hicho
na kutoa misaada mbalimbali kwa wagojnwa waliolazwa kituoni hapo ikiwa
ni kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...