Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia),
akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama, wakati wajumbe hao walipotembelea eneo litakalojengwa Jengo la Makao
Makuu ya Uhamiaji, Jijini Dodoma, leo. Ujenzi wa jengo hilo ambao tayari
umenza, unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 16. Katikati aliyevaa kofia ni
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Victor Mwambalaswa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,
Ulinzi na Usalama, Ramadhan Abdallah, akitoa taarifa ya Kamati hiyo, katika
kikao chao na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Kushoto meza
kuu ni Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola. Katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa
Kamati hiyo, Victor Mwambalaswa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto),
na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (katikati),
wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala,
alipokuwa anawafafanulia jambo katika eneo la ujenzi wa Makao Makuu ya Idara
hiyo, jijini Dodoma, leo. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia),
akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama, katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, Jijini
Dodoma, leo. Mara baada ya kikao hicho, wajumbe hao walitembelea eneo
litakalojengwa Jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji, Jijini Dodoma. Ujenzi wa jengo
hilo ambao tayari umenza, unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 16. Kulia ni
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Victor Mwambalaswa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...