Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akifafanua jambo katika kikao cha Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Bungeni, jijini
Dodoma leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Kulia ni
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akifurahia jambo wakati alipokua
anazungumza na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama, Victor Mwambalaswa, na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, Prosper Mbena, wakati walipokua wanatoka katika kikao cha
Kamati hiyo, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mussa
Zungu (kushoto meza kuu), akiwa na wajumbe wa kamati hiyo, wakimsikiliza Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani) alipokua akifafanua jambo katika
kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo. Waziri Lugola aliambatana
na Watendaji Wakuu wa Wizara yake katika kikao hicho.
Naibu Katibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (kushoto)
akifurahia jambo na Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel, mara baada ya Naibu Katibu
Mkuu huyo kutoka katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...