Hitimisho
la Wiki ya Maji Duniani, Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka (DAWASA)
wamewapa furaha wakazi wa Saranga na maeneo jirani kwa kuwapatia maji
safi na salama.
Akizungua wakati wa kuzindua mradi wa kuwasambazia maji wakazi wa
Saranga Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori
amesema kuwa amefurahishwa jinsi DAWASA walivyoweza kuwapa furaha wakazi
hao wa Saranga kwa kuwapatia maji ambayo watakuwa wakiyapata masaa 24.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es S alaam Kisare Makori (kushoto)
akimpongeza Kaimu Mkurugenzi wa miradi DAWASA Lydia Ndibalema kwa kuweza
kufanikisha uwekaji wa bomba eneo la Saranga jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori (kushoto)
akimpongeza Kaimu Mkurugenzi wa miradi DAWASA Lydia Ndibalema kwa kuweza
kufanikisha uwekaji wa bomba eneo la Saranga. Wengine wa kwanza kushoto
ni
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori (kushoto) akizungumza na wakazi wa Saranga (picha ya chini)
Kaimu Mkurugenzi wa miradi DAWASA Lydia Ndibalema akizungumza na wakazi
wa Saranga jijini Dar es Salaam kuwaelezea jinsi walivyoweza kufanikisha
kufikisha mradi huo.
Meneja
wa DAWASA- Kimara jijini Dar es Salaam Paschal Fumbuka akielezea jinsi
mradi ulivyoweza kukamilika wakati wa hitimisho la wiki ya Maji Duniani
iliyoanza Machi 16-22, 2019.
Diwani wa kata ya Saranga Mhe. Haruni Mdoe akizungumza na wakazi wa Kimara Tembeni kata ya Saranga jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori (wa tatu kutoka
kushoto) akikata utepe na Diwani wa kata ya Saranga Mhe. Haruni Mdoe
kuzindua huduma hiyo.
Tukio
Lingine alilolifanya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Makori ni kuzindua
eneo la Bomba la Kwanza lililowekwa kwa mkazi mmoja wa Saranga ili
kuonyesha ishara ya usambazaji wa maji kwa wakazi hao.
Wakazi wa Saranga wakijiandikisha mbele ya wenyekiti wa Serikali za mtaa ili waweze kupatiwa maji na DAWASA.
Meneja
wa huduma kwa wateja wa DAWASA Doreen Kiwango akiangalia zoezi la
uandikishaji wateja wapya wakazi wa Saranga linavyoendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...