MWANAMUZIKI wa kizazi kipya mwenye uwezo mkubwa wa kuteka hisia za mashabiki Amini Mwinyimkuu anatarajia kuipua kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Nimenasa akimshiriki mwanadada aliyekwe ubora wake Esterina Peter Sanga a.k.a Linah.
Akipiga stori na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam Amin amesema wimbo huo utauachia wiki ijayo na kwamba ameufanyia Studio ya C9 chini ya mtayarishaji Kichwa Touch Killer.
Kama kawaida yake akiwa anazungumza kwa upole wa hali ya juu ukiambatana na umakini wa kujieleza amesema ni wakati muafaka wa kutoa wimbo huo akiwa amemshirikisha Linah kwani ni mwanamuziki wa kike anayemkubali.
Ujue iko hivi Amini na Linah huko nyuma walikuw na uhusiano ule wa kibaba na mama lakini safari hii wameamua kukutana kwa ajili ya kufanya kazi moja tu ya kutoa wimbo kwa ajili ya mashabiki wao.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wao wa kimapenzi kama wameruadia au laa, Amini akizungumza kwa kujiamini kama jina lake kuwa hakuna uhusiano huo zaidi ya ule wa kufanya kazi kama wasanii.
"Hatuna uhusiano ila nimeamua tu safari hii katika wimbo wangu mpya nishirikiane na dada Linah."Swali likawa tena kwanini Amini anamuita dada Linah ,eti akajibu hivi "Wanawake ndio mama zetu, na akiwa mdogo kwangu atakuwa dada,ndio maana nasema ni dada Linah."
Kwanini ameamua kumshirikisha Linah katika kibao hicho cha Nimenasa, amejibu anavutiwa na uwezo na kipaji cha mwanadada huyo na kwamba Linah hata akiamshwa kutoka usingizi ubora wa sauti na uwezo wa kuimba uko palepale.
"Linah anao uwezo mkubwa sana wa kuimba na ndio maana nimeamua kumshirikisha,pia na hata pale unapokuwa umetunga mashairi ya wimbo ukimpa anaweza kukariri kwa muda mfupi," amesema Amini.
Alipoulizwa kama Caple yao yaani Amini na Linah inaendana ,amejibu ukweli ni kwamba mashabiki wanaofuatilia muziki wao wamekuwa wakisema wanafurahia Caple yao na wanatamani wafanye kazi pamoja.Mbona raha.Acha tusubiri tuone kama kweli wanaweza kuishia kwenye kuimba tu au watarudi kuleee kwenye mahusiano ya michezo ya kibaba na kimama.
Kwa kukumbusha tu msanii Amini umaarufu katika muziki umetokana na nyimbo zake mbalimbali zikiwemo Ni wewe,Mtima wangu, Robo Saa, Unikimbie, Nyota,Yameteka dunia na Novemba or Desemba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...