
Akizungumza katika Mkutano wa kuwapokea Madiwani hao Katibu wa HKT Mwenye dhamana ya Itikadi na Uenezi Ndg. H. Polepole amesema tofauti na nyakati nyingine awamu hii ya tano ya Uongozi wa Chama na Serikali chini ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli tumejifunza kwamba iko tija kubwa katika kusema na kisha kutenda.
Ndg. Polepole ameelezea miradi mikubwa ya kimkakati na miradi mikubwa ya kisekta ikiwemo Elimu bure, Huduma za Afya, Barabara, Maboresho makubwa ya Kilimo na Upatikanaji wa maji inatekelezwa kwa haraka na asilimia kubwa ikiwa fedha za ndani.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatoa Maelekezo kwa Serikali kwamba ifikapo Julai 1, 2019, taasisi ndogo ndogo binafsi zinazojihusisha na utolewaji wa huduma za Maji zitakuwa chini ya Mamlaka ya Serikali ili kuongeza ubora, ufanisi na kushusha viwango vya bei za maji kwa wananchi ikiwemo hapa Karatu kwasababu jambo hili jema na ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM amesema Ndg. Polepole
Shughuli ya kupokea Madiwani Wilayani Karatu imehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Ndg. Loata Sanare, Mjumbe wa HKT Mkoa wa Arusha Ndg. Daniel Awaki na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Karatu.
Huu ni muendelezo wa kazi za ujenzi na uimarishaji wa Chama ndani ya Chama na nje ya Chama ndani ya Jamii ikiwemo kujiridhisha utekelezwaji wa Ilani ya CCM.
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...