Naibu meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Joseph Lyata kupitia chama cha mapinduzi akikagua utekelezaji wa ahadi waliyoitoa kwa wananchi wa kata ya Mkimbizi mtaa wa Ugele manispaa ya Iringa
Naibu meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Manispaa ya Iringa Edwin Bashir pamoja na mwenyekiti wa vijana kata ya Mkimbizi wakikagua utekelezaji wa ahadi yao
Naibu meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Manispaa ya Iringa Edwin Bashir pamoja na diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula wakifurahi jambo na wananchi wa mtaa wa Ugele mara baada ya kutekeleza ahadi ya ujenzi wa barabara
Naibu meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Manispaa ya Iringa Edwin Bashir pamoja na diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula wakifurahi jambo na wananchi wa mtaa wa Ugele mara baada ya kutekeleza ahadi ya ujenzi wa barabara


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

NAIBU meya wa manispaa ya Iringa amewataka wananchi wa manispaa ya Iringa kumkataa mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wa kuleta maendeleo kwa wananchi waliompa kura.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Mkimbizi mtaa wa Ugele,Naibu meya Joseph Lyata alisema kuwa mfuko wa mbunge unapesa nyingi za kusaidia kuleta maendeleo kwa wananchi lakini hali imekuwa tofauti kwa mbunge huyo kushindwa kutatua changamoto za wananchi.

“Mbunge anauwezo wa kuwatembelea wananchi wa Ugele na kuja kutatua changamoto mlizonazo kwa kuwa anapesa za mfuko wa mbunge ambao anauwezo wa kutoa pesa kwa ajili ya kukarabati barabara hii ambayo imekuwa kikwazo kikubwa katika kuleta maendeleo ya eneo hili” alisema Lyata

Lyata alisema kuwa wananchi wa mtaa wa Ugele wanakabiliwa na tatizo la kukosa huduma bora za afya kwa kuwa mbunge wa jimbo hilo hayupo tayari kuwasaidia kutatua changamoto hizo.

“Mlifanya kosa kubwa sana kumchagua mbunge huyo kwa kuwa hajawai kuja kuwasikiliza kero zeo na kuzitatua ndio maana maumivu hayo mnayapa hii leo kwa kuwa hakuna maendeleo ambayo mmefanyiwa na mbunge huyo” alisema Lyata

Lyata amewataka wananchi wa mtaa wa Ugele kutomchagua tena mbunge huyo kuwa kuwa hana faida ya kimaendeleo kwa wananchi kwa kuwa ameshindwa kuleta maendeleo kwa kushindwa kuboresha sekta ya afya,elimu na miundombinu.

“Mmemchagua kiongozi ambaye hawasikilizi na anashindwa kutatua kero za wananchi ndio maana hadi hii leo mnateseka kwa kushindwa kutatuliwa kero zenu huyo sio kiongozi na hafai tena kuwa kiongozi” alisema Lyata

Aidha Lyata alisema kuwa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa kimeamua kutatua kero zenu kwa kuwa hamna kiongozi ambaye anaweza kuwatatulia kero kwa kuwa mbunge mliyemchagua ameshindwa kutatua kero hizo.Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Manispaa ya Iringa Edwin Bashir aliwataka wananchi wa mtaa huo kuendelea kuwa na imani na chama cha mapinduzi kwa kuwa kinafanya kazi ya kuleta maendeleo kwa vitendo.

“Tulikuja hapa kukiwa hakuna barabara lakini tulifanya mkutano wa hadhara na kuwasikiliza kero zetu hatimaye mkatupa kero ya barabara na zahanati hivyo sasa tumeanza kutengeza barabara kwa kiwango bora kinachosaidia kuleta maendeleo kwa wananchi” alisema Bashir

Bashir alisema kwa sasa hakuna chama kinachoweza kutekeleza ahadi zake kwa umakini kama chama cha mapinduzi hivyo wananchi mnatakiwa kuendelea kuwa na imani na chama hicho.“Jamani mnatakiwa kuendelea kukienzi na kukitunza chama hiki bora ambacho ndio chama bora kwa kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wake na sio vyama vingine” alisema Bashir

Kwa upande wake diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula alisema kuwa chama cha mapinduzi na naibu meya wa manispaa ya Iringa walikuwa hawalali kwa ajili ya kutatua tatizo la barabara ya Ugele kwa kuwa wananchi hao wanahitaji kufanya kazi za kimaendeleo

“Wananchi wa kata ya Ugele wanahitaji kufanya maendeleo kwa kuwa wamekuwa wachapa kazi wakubwa lakini mbunge wao amekuwa hawasaidie kwa lolote hivyo ndio chama na Naibu Meya walipobebe jukumu la kutatua changamoto hiyo” alisema Chegula

Chegula alisema kuwa kipaumbele kilikuwa kutatua changamoto ya barabara ndipo wanatafuta njia nyingine ya kutatua changamoto nyingine zilizopo katika mtaa wa Ugele ili wananchi wafanye kazi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyotaka.

Nao wananchi wa Mtaa wa Ugele Manyigi Uliopo Kata ya Mkimbizi Manispaa ya Iringa wameishukuru serikali Chini ya Naibu Meya Manispaa ya Iringa kwa kuwakarabatia barabara ambayo ilikuwa awali ilikuwa kero kwao.

“Baadhi ya wananchi wa Mtaa huo wamesema kuwa awali kabla ya ukarabati wa barabara hiyo, wajawazito walikuwa wanapata shida pindi wanapoelekea mjini kupata huduma za afya” walisema wananchi

Mwenyekiti wa Mtaa wa Ugele Manyigi Aloyce Laurent amemshukuru Naibu Meya Joseph Lyata kwa kupeleka Greda katika Mataa wake na kurekebisha barabara ambayo ilikuwa kero kwa wananchi wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...