Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na waandishi mbalimbali ofisini kwake juu ya kusambaa kwa habari ambayo ilitungwa na mtu mmoja.



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Siku chache baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa ameshika viungo bandia vya kiume na kuzua Taharuki katika jamii, Mkuu huyo wa Wilaya ametolea ufafanuzi.

Akizungumza na Wandishi wa habari ofisini kwake leo Kasesela amesema kuwa taarifa zilizosambaa mtandaoni juu ya uzalishaji wa viungo bandia vya kiume, zimeleta changamoto huku akiwataka wananchi kuondokana na dhana potofu za kuchukua habari za mitandaoni na kuupotosha umma.

“Naomba niendee kuwaomba radhi watanzania kwa ajili ya jambo ambalo lilileta taharuki kwenye mitandao ya kijamii hasa nchi ya jirani zetu hapo Kenya lilipokelewa tofauti na nilivyokuwa hapo awali” alisema Kasesela 

Kasesela aliwataka watanzania kuacha kufuatia mambo ya ajabu na kuyapa nafasi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kupata mambo ya kujenga nchi na yenye tija.

“Jamni ile habari ilitungwa na ni habari ya hovyo sana kwa kuwa nililishwa habari ambayo mimi sijaisema kwenye chombo chochote kile kwenye vyombo vya habari hivyo hiyo habari ni ya kupuuza tu” alisema Kasesela

Kasesela amewashauri watanzania kuhakikisha wanafatilia taarifa zenye kuleta maendeleo na zenye kujenga katika jamii inayomzunguka.“Kwa sasa habari nyingi ambazo zinazungumzwa hivi sasa ni habari ambazo ni za hovyo hovyo mno ndio maana leo wamesema kuwa wilaya ya Iringa kuna kiwanda hicho kitu ambacho sio kweli” alisema Kasesela .

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela amelaani kitendo cha Dawson Kagine kusambaza taarifa zisizo za kweli na kuongeza kuwa mkoani Iringa kuna kiwanda cha kuzalisha vifaa vya elimu ya mapambano dhidi ya Ukimwi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...