Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, (CGF) Thobias Andengenye, amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa hapa nchini.

Makamanda walioguswa na mabadiliko hayo ni Kamishna Msaidizi wa Zimamoto (ACF) Mohamed Kondo, aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kinondoni, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya.

Kamishna Msaidizi (ACF) Juma Yange, aliyekuwa Kitengo cha Utawala Mkoa wa Kinondoni, anakuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kizimamoto Kinondoni.

Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) John Francis, aliyekuwa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Handeni Mkoani Tanga, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Rukwa.

Vilevile, aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma, Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) Athumani Basuka, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Hai – Siha, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) Jumbe Juma.

Pia aliyekuwa Kamanda wa Kiwanja cha Ndege Mkoa wa Iringa, Mkaguzi wa Zimamoto (INSP) Hamisi Dawa, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kagera. 

Mabadiliko haya ni ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea kutoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Makamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mikoa na Wilaya katika suala la Kinga na Tahadhari Dhidi ya majanga.

Imetolewa na;
Joseph Mwasabeja – (INSP)
Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Makao Makuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...