MABONDIA Hussein
Pendeza na Juma Ramadhani 'Choki' wametamba kila mmoja kwa wakati wake kuibuka
na ushindi katika mpambano kati yao ambao unatarajia kufanyika Aprili 21 mwaka
huu ambayo itakuwa Sikukuu ya Pasaka.
Akizungumzia mpambano
huo ambao utafanyika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu uliopo Magomeni Mapipa jijini Dar
es Salaam Juma Ramadhan 'Choki' amesema ana uhakika wa kushinda kwani hivi sasa
yupo fiti mpaka mwenyewe anajiogopa kutokana na mazoezi ambayo ameyafanya
kujiandaa na pambano hilo.
"Kwa namna
ambavyo nimejiandaa , sio huyo tu Pendeza, yoyote ambaye atakuja mbele yangu
atapokea kichapo tena cha mbwa mwizi.Hivyo wakae chonjo vingenevyo
nitawararuaraua na sijaona katika uzito wangu wangu wa kilogramu wa kunisumbua
kwani najiamini na ninajimini kwa mazoezi ambayo nimeyafanya,"amesema.
Hivyo Choki amewaomba
mashabiki wake wa Manzese,Mabibo, Mbagala Kuu na Mtoni Kijichi kujitokeza kwa
wingi siku hiyo ili kumpa sapoti na anataka kuweka historia ya aina yake kwenye
mpambano huo.
Kwa upande wake bondia Pendeza amesema kuwa atahakikisha
anampiga Choki kama begi kwani kwake ni mtoto mdogo sana katika ulimwengu wa
masumbwi na kipigo ambacho atampatia atajuta kuzaliwa kwa kipigi ambacho
atakipata.Pia ameongeza anawaomba mashabiki wake wote na wapenzi wa ngumi
kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuangalia jinsi anavyo msambaratisha mpinzani
wake.
Mpambano huo
umeandaliwa na Promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo
amefafanua maandalizi yote muhimu yameshafanyika ."Pambano litafanyika
Siku ya Sikukuu ya Pasaka,"amesema Super D.
Pia amesema bondia mtanzania
Omari Kimweri 'Lion Boy 'anayefanya shughuli zake nchini Australia ndiyo
aliyosababisha mabondia hao wazipige siku hiyo kwa kuwa vijana wanatakiwa
kuendeleza rekodi zao za masumbwi kila wakati ndio maana akaongeza nguvu ili
mpambano uho ufanyike
Super D ameongeza
mbali na pambano hilo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine yatakayokuwa
yanafanyika siku hiyo ambapo bondia Idd Mkwera ataoneshana umwamba na
Rojas Masamu wakati Shomari Milundi ataoneshana umwamba na Bakari Mbede.
Wakati Ibrahimu Makubi
atavaana na Haruna Ndalo na Ramadhani Mbegu 'Migwede' atapambana na Rashidi
Mnyagatwa na Salum Tandu zidi ya Gerald Mkude na Sunday Kiwale 'Moro Best'
atalindima na Luckman Ramadhani Vicent Mbilinyi na Shabani Mbogo Hussein
Shemdoe na Shehe Azizi na Ahmadi Kombo atakumbana na Sandali Nyambala
Mapambano yote hayo
yanaletwa yanafanyika chini ya kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing
Promotion ambayo ipo nchini Tanzania kwa ajili ya kuinua vipaji ya vijana
mbalimbali ili kuendeleza vipaji vyao pendwa na kupitia kampuni ya Super D
Promotion imejizatiti kuweka angalau pambano moja kila baada ya miezi milili ili
kuwasaidia vijana kukuza vipaji vyao na kujiendeleza kupitia mchezo uho wa
masumbwi nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...