Na Bakari Madjeshi wa Michuzi TV 
Mkazi wa Singida, Mariam Rajab Juma anayesumbuliwa na tatizo la kidonda kikubwa kilichopo sehemu ya mgongoni ameeleza kuwa tatizo hilo chanzo chake kilianzia kwenye Jipu ambalo baadae lilipasuka nakupelekea kidonda hiko. 

Mariam aliyelazwa kwa ajili ya matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) amezungumza hayo alipokuwa akihojiwa na Waandishi wa Habari hospitalini hapo. 

Mariam ameeleza kuwa tangu kufika Muhimbili ameona kuna mabadiliko makubwa, amesema kwa sasa anatembea vizuri tofauti na zamani.

"Naishukuru Serikali na Watanzania kwa ujumla kwa hali niliyonayo sasa, kuna mabadiliko makubwa tangu tatizo hili lianze miezi Saba iliyopita", amesema Mariam.

Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Upasuaji na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma amethibitisha kuwepo kwa Mgonjwa huyo takriban wiki moja iliyopita, amesema wamefanya uchunguzi kwa Mariam nakujiridhisha kile kinachomsumbua. 

Dkt. Mkoma amesema baada ya upembuzi yakinifu kuhusu kinachomsumbua Mariam, ataendelea na matibabu katika hospitali ya Ocean Road kwa muda na baadae atafanyiwa uchunguzi tena na Jopo la Madaktari. 

Amesema baada ya uchunguzi huo, Jopo hilo la Madaktari litakaa tena kufanya tathmini kujua anaendelea na matibabu ya aina gani. 

Kuhusu tatizo zaidi lilonalomsumbua Mariam, Dkt. Mkoma amesema suala hilo litabaki kuwa siri kati ya Madaktari na Mgonjwa.

Hata hivyo, Dkt. Mkoma ametoa wito kwa Wananchi kuwa na tabia yakuchunguza afya mara kwa mara, amesema inapokea kuwa na kidonda chochote kwenye kovu la zamani lazima kufanya kipimo kujua ni aina gani ya kidonda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...