NaTheresia Mallya - Afisa Habari Tunduru DC




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ametoa maagizo kwa waziri wa Tamisemi Mhe.Selemani Jafo kutoa shilingi milioni 200 za kukamilisha ujenzi na upanuzi wa  kituo cha afya Juma Homera kilichopo Nakayaya wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.

Maagizo hayo ameyatoa wakati akitoa hotuba kwa wananchi wa wilaya hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya soko la Mchele –Nakayaya akiwa katika ziara ya kikazi siku ya pili mkoani Ruvuma.

Rais Magufuli alifikia uamuzi huo baada ya kuguswa na michango ya wananchi waliotoa katika kuchangia ujenzi wa kituo cha afya Juma Homera ya shilingi Milioni 189 ili kujenga kituo hicho kitakachosaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya
Tunduru.

“Waziri wa Tamisemi nakuagiza ulete shilingi milioni 200 kwa ajili ya kufanya upanuzi wa kituo cha afya Juma Homera ili kitoe huduma za upasuaji,mionzi,kuongeza wodi za kutosha ili kurahisha huduma za afya kwa wananchi wa Tunduru”

aidha katika hatua nyingine Rais Magufuli Alimuagiza waziri wa Tamisemi Selemani Jafo kutoa shilingi milioni 500 za ujenzi wa kituo cha afya katika Kata ya Namiungo ambayo haina zahanati wala kituo cha Afya katika vijiji saba vya kata hiyo.

Magufuli alilazimika kusimamisha msafara na kuwasikiliza wananchi waliokuwa wamefunga barabara ambapo alisema kuna kila sababu ya kata hiyo kuwa na kituo bora na cha kisasa ili kupunguza vifo vya kinamama na wajawazito na watoto vinavyosababishwa na kusafiri umbali mrefu
kufuata huduma za afya.

Hata hivyo alimaliza kwa kuwataka wananchi kufanya kazi na kushikamana katika kuijenga Tunduru na kuepuka chuki za kisiasa kwani  maendeleo hayana chama, niwatake wanatunduru muungane kwa pamoja katika kuleta maendeleo chanya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...