Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu akiwasha Mwenge wa Uhuru
kuashiria uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa Mwaka 2019,
Mkoani Songwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu akihutubia wananchi wa
Songwe walioshiriki kwa wingi katika uwanja wa Kimondo – Forest,
Wilayani Mbozi kushuhudia uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa
kwa Mwaka 2019.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Mkoa wa
Songwe waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Songwe
walioshiriki kwenye hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa
kwa mwaka 2019.
Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa
na Michezo wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Balozi Ali Karume akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye Uwanja wa
Kimondo, Wilayani Mbozi Aprili 2, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela akieleza jambo kuhusu Mkoa wa Songwe.
Sehemu ya Vijana wenye dhamana ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 (waliosimama mstari wa mbele).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu akiwa pamoja na Waziri
Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakifuatilia matukio ya vijana halaiki.
(Kulia) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Kushoto) ni Waziri
wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Zanzibar, Mhe.
Balozi Ali Karume.
Vijana wa Halaiki wakionesha picha
ya Mwl. Julius K. Nyerere wakati wakiimba nyimbo ya kumsifu kwenye
hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu akimkabidhi Mwenge wa
Uhuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bw. Mzee Mkongea Ali.
(Kulia) ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia
Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bw. Mzee Mkongea Ali baada
ya kukabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Hassan Suluhu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge
zilizofanyika Aprili 2, 2019 Mkoani Songwe katika Uwanja wa Kimondo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama pamoja na Viongozi mbalimbali walipokuwa wakicheza na kufurahi
wakati wanakwaya ya JKT Mlale walipokuwa wakiimba nyimbo na kutoa
burudani kwa wananchi wa Songwe waliohudhuria uzinduzi wa Mbio za Mwenge
wa Uhuru.
Baadhi ya wananchi wa songwe
wakifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu (hayupo pichani). Makamu wa Rais
alikuwa Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru Kitaifa Mwaka 2019.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
…………………………
Na OWM (KVAU) – SONGWE
Serikali imedhamiria kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi waishio mijini kufikia asilimia 95 na vijijini asilimia 85 ifikapo 2020.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama Samia Hassan Suluhu wakati wa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Aprili 2, 2019 zilizofanyika uwanja wa Kimondo – Forest Mlowo, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe.
Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2019 isemayo “Maji ni Haki ya kila Mtu, Tutunze Vyanzo Vyake na Tukumbuke Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”
Makamu wa Rais amesema kuwa dhamira ya Serikali inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ni kuboresha huduma za jamii ikiwemo sekta ya elimu, afya, barabara, umeme vijijini, usafiri wa anga, uvuvi, kilimo, viwanda na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wote.
“Sera yetu ya Maji ya mwaka 2002 inasisitiza upatikanaji wa maji safi na salama ambayo ni muhimu kwa maisha ya kila mtu, shughuli za kiuchumi na ustawi wa mazingira,” alisema Makamu wa Rais.
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa maji safi, alieleza kuwa Serikali inaendelea kutekeleza ujenzi wa miradi mbalimbali ya maji nchini ikiwemo mabwawa ya kimkakati na kuboresha miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji safi.
Aidha, Makamu wa Rais alitoa wito kwa Wananchi kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji kwa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kando ya vyanzo hivyo.
Kupitia hadhara ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Makamu wa Rais, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao ni muhimu katika kuleta maendeleo ya watu na huduma za kijamii.
Awali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alisema kuwa Mwenge wa Uhuru ndio msingi mkubwa wa amani, Mshikamano, Uzalendo na Umoja tulionao katika Taifa.
“Tunu hii imekuwa ni kichocheo cha maendeleo kwa wananchi na wamekuwa wakihamasika kushiriki katika kuandaa na kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo ya kijamii na kiuchumi iliyopo katika maeneo yao,” alisema Mhagama.
Waziri Mhagama aliongeza kwa kuwashukuru wadau mbalimbali waliosaidia kufanikisha tukio hilo muhimu la Kitaifa.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela alishukuru Serikali kwa kuchagua Mkoa wa Songwe kuwa wenyeji wa Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2019.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...