Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
ILI kuhakikisha nchi inafikia katika na uchumi wa kati na wa viwanda ifikapo mwaka 2025, serikalo  kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta binafsi nchini, (TPSF) imeweka mkakati wa kuanzisha, kusimamia na kuratibu mabaraza ya ujuzi kisekta kwa lengo la kuendeleza ujuzi katika sekta mbalimbali.

Imeelezwa kuwa ili kufikia malengo hayo kuwapo kwa nguvu kazi yenye ujuzi stahiki in suala ambalo halikwepeki na serikali inawekeza nguvu na rasilimali nyingi kwenye maeneo yenye  kipaumbele ambapo amesema ipo mikakati mbalimbali ya taifa ya kuendeleza ujuzi na wa  kukuza stadi za kazi na ujuzi ambayo ina programu nne.

Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bahati Geuzye kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo ameyasema hayo leo Aprili    wakati akifungua warsha ya kuwajengea uwezo wadau kuhusu mabaraza ya ujuzi kisekta,.

Amesema, Program hizo ni Mfuko wa kukuza stadi za kazi na ujuzi, Ujuzi vocha, mabaraza ya ujuzi ya Kisekta na kuwajengea uwezo taasisi zinazotekeleza miradi. Ambapo sekta ambazo zimepewa kipaumbele katika program hiyo ni Kilimo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Nishati, Ujenzi, Uchukuzi na Utalii.

Amesema, mhango (TPSF), utasaidia kuanzisha, kusimamia na kuratibu mabaraza ya ujuzi kisekta. Ambayo yatakuwa kiunganishi muhimu kwa kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wa masuala ya kuendeleza ujuzi nchini,.

Aliongeza kuwa serikali inategemea ushirikiano kutoka kwa wadau wa sekta binafsi ili kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati na kwamba wanapaswa kushiriki katika program za uanagenzi, mafunzo ya wahitimu tarajali mahali pa kazi na kutambua ujuzi uliopatikana  nje ya mfumo rasmi wa elimu ili kusaidia kupunguza tatizo la ujuzi nchini

‘"Serikali itaendelea kutoa ushirikiano katika kusaidia jitihada za sekta binafsi na wadau wengine kuweka sera, program mbalimbali za kuendeleza ujuzi, kuimarisha miundombinu na kuweka mazingira wezeshi ili kuvutia wawekezaji,’’ amesema Gauzye

Pia alieleza, serikali inatambua kwamba sekta binafsi ndio injini ya ukuaji wa uchumi nchini na kwamba itafanya kila linalowezekana kuiwezesha sekta binafsi katika kukuza ujuzi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema, Tanzania ni nchi ya kwanza katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuwa na mkakati wa kuongeza ujuzi ambao ni wa miaka 10 kutoka 2016 hadi 2026.

‘’Kwa miaka mingi waajiri wamekuwa wakipata changamoto kubwa ya kupata rasilimali watu wenye ujuzi unaohitajika katika kutekeleza majukumu yao. Changamoto hii imekuwa ikisababisha kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa biashara,’’ alisema Simbaye.

Aliongeza kuwa ‘’waajiri hulazimika kutafuta wataalamu wenye ujuzi stahiki kutoka nje ya nchi au kutumia gharama kubwa kugharamia mafunzo kwa watumishi katika sehemu zao za kazi, hivyo mradi huo ni muhimu kwetu tutahakikisha tunautekeleza kwa ufanisi mkubwa kwa maslahi mapana ya waajiri na taifa kwa ujumla.’’

Alisisitiza kuwa TPSF na Wizara ziliingia makubaliano Machi mwaka jana na utekelezaji wake ulianza Februari mwaka huu baada ya kuwezeshwa fedha na serikali ambapo awamu ya kwanza ya utekelezaji, TPSF ilianza kuwajengea uelewa wadau mbalimbali kutoka sekta za kilimo, utalii na usafirishaji, wakurugenzi wa kampuni, vyama vya biashara na wahariri wa vyombo vya habari na katika awamu ya  pili ya uanzishwaji wa mabaraza haya tutaajirlli watumishi wa mabaraza, kutenga eneo la ofisi kwa ajili ya watumishi wa mabaraza, kununua vifaa na vitendea kazi mbalimbali vya ofisi na kuunda na kuteua wajumbe wa mabaraza,’’ alisema.
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bahati Nguze akitoa hutuba kwa niaba yabKatibu Mkuu wa Wizaravya Elimu Sayansi Teknolojia Dr. akwilapo wakati wa warsha ya siku moja juu ya masuala ya ujuzi wa sekta binafsi nchini.
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bahati Nguzye mwenye shati jeupe,  mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Godfrey Simbeye,  wa Kati kati wakifuatilia  warsha ya siku moja juu ya masuala ya ujuzi wa sekta binafsi nchini. Wa kwanza Kulia Edward Furaha,  mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wizara ya Elimu na kushoto ni Osward Rukonge Mratibu Msaidizi wa mradi wa ESPS Wizara ya Elimu.
Baadhi ya wadau kutoma sekta binafsi na Serikalini wakifuatilia majadiliano wakati wa warsha ya siku moja juu ya masuala ya ujuzi wa sekta binafsi nchini iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...