Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
ASKARI wa jeshi la polisi mkoani Pwani, wanakabiliwa na tatizo kubwa
la ukosefu wa makazi ya kuishi, hali inayosababisha kushindwa kuwahi
wakati wakihitajika haraka katika dharula za majukumu yao ya kikazi.
Kutokana na hali hiyo, kwasasa jeshi hilo linajenga nyumba 20 za
makazi ya askari polisi hao,zitakazogharimu milioni 500 ili
kukabiliana na hali hiyo.
Akizungumza wakati alipokwenda kutembelea ujenzi wa nyumba hizo
zinapojengwa Kibaha Mjini, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama
mkoani Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alitaka ujenzi huo ,ukamilike
ifikapo June 30 mwaka huu, kama amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi na
usalama ,dkt. John Magufuli alivyoelekeza.

Alisema ,askari wanapaswa kulinda mali ya mwananchi na kulinda usalama
wa raia hivyo wanatakiwa waishi kwenye mazingira yaliyo bora.
"Kanda maalum ya kipolisi Rufiji imepatiwa milioni 500, pamoja na
jeshi la polisi Pwani milioni 500, jumla milioni 100, ambazo
zimetolewa na serikali kuhakikisha kila mkoa askari wanajengewa makazi
ya kuishi "
"Hivyo ni wajibu wa jamii, wenye viwanda kushirikiana na serikali na
jeshi la polisi kujenga mazingira bora ya askari hawa waweze kutulinda
kwa moyo na upend "alifafanua Ndikilo.

Awali akitoa taarifa fupi kwa mkuu wa mkoa huyo juu ya ujenzi
unavyoendelea, kamanda wa polisi Pwani, Wankyo Nyigesa alibainisha,
kutokana na ufinyu wa bajeti wamepewa milioni 500 na kwa wastani kila
nyumba itagharimu milioni 25 mpaka kukamilika kwake.
Aliwashukuru wadau waliojitokeza kusaidia akiwemo Said Salim Bakhresa,
jeshi la wananchi wa Tanzania kupitia kikosi cha usafirishaji (KJ 95)
ambao waliwapatia lowbed kwa ajili ya kubeba buldoza kutoka bakhresa
sugar company huko Bagamoyo.
Wengine ni Chila mkurugenzi wa Creative Intertraders ltd ambae ametoa
mifuko 100 ya saruji na Twyford Ceramics (KEDA )ya Chalinze na wengine
ambapo amewashukuru na kuomba wadau wengine waendelee kuwashika mkono.
Mkoa wa Pwani ni moja ya mikoa ambayo , Amiri Jeshi wa Majeshi dk.
Magufuli akiwa anazindua nyumba za askari polisi mkoani Arusha ,april
7 mwaka 2018, alitoa maelekezo kwa mkuu wa jeshi la polisi nchini
(IGP) kwamba atapatiwa fedha kwa ajili ya makazi ya askari ,ambapo
mkoa huo umeanza utekelezaji baada ya kupokea fungu hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...