Kutokana na utabiri uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kuhusu kutokea kwa Kimbunga kikali (KENNETH) na mvua kubwa leo tarehe 25 Aprili 2019 kitakachoathiri maeneo ya Pwani ya Kusini mwa nchi na kusababisha madhara mbalimbali. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatoa rai kwa Wananchi wote waishio katika maeneo hatarishi, maeneo yaliyopo pembezoni mwa bahari na kandokando ya Mito, kuchukua tahadhari katika kipindi hiki kwa kuyahama maeneo hayo haraka.

Wananchi wanatahadharishwa kuchukua tahadhari katika kipindi hiki na kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania na kusikiliza vyombo vya habari pamoja na kuzingatia tahadhari zinazotolewa, ushauri na miongozo ya kitaalam ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Tuchukue tahadhari kwa kuepuka kukaa au kuegesha vyombo vya Usafiri na Usafirishaji chini ya miti mikubwa, maana matawi au mti vyaweza kuangukia chombo na kusababisha uharibifu mkubwa wa Mali hata kudhuru Maisha.

Kutokana na Kimbunga hiki kikali kinachoambatana na mvua kubwa kuna uwezekano wa mawe makubwa au udongo kuporomoka kutoka milimani au miti kuanguka na kuziba barabara, hivyo madereva wanapaswa kuwa makini kwa kuendesha vyombo kwa mwendo unaokubalika ili kuepuka ajali zisizo za lazima.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limejipanga na liko imara kuhakikisha linatoa huduma bora, sahihi na kwa wakati.

Imetolewa na;
Billy Mwakatage
Kamishna wa Operesheni
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...