Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, na uzuiaji wa wanyama pori na ndege hai leo wameshiriki katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utendaji katika Viwanja vya Ndege yaliyoandaliwa na KOICA (Korea International Cooperation Agency) na kutekelezwa na wataalam kutoka Kiwanja cha Ndege cha Incheon kilichopo Korea Kusini ambacho kinaaminika kuwa na ubora nambari moja katika nyanja ya usalama na uendeshaji duniani.
Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa watu mashuhuri Katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jengo la pili la abiria (TB II), ikiwa ni mwendelezo wa mpango wa mafunzo ya miaka mitatu kwa watendaji wa TAA na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA).
Akitoa maelezo kuhusu mafunzo hayo Meneja wa Mafunzo kutoka Kiwanja cha Ndege cha Incheon Bi. Ji-Yoon Park ameeleza kwamba mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo ya awali ambapo kwa awamu ya kwanza Mafunzo yalitolewa kwa watendaji takribani 15 kutoka TAA na ZAA na mafunzo haya ni sehemu ya mpango wa mafunzo ya miaka mitatu (2018 – 2020).
Mafunzo haya yatafanyika kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 15 Aprili na yatamalizika siku ya kesho16 Aprili nakuendelea huko Zanzibar ambapo yatafanyika katika Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar.
Katika awamu ya kwanza ya mafunzo haya yalifanyika mwezi Septemba mwaka jana na Watendaji kumi na tano (15) walinufaika na mafunzo haya ikiwa ni (10) kutoka TAA na watendaji na watano (05) kutoka ZAA.
Ikumbukwe kuwa TAA na ZAA mnamo Juni 2018 waliingia katika makubaliano na KOICA ya kutoa mafunzo kwa Watumishi kwa muda wa miaka mitatu ambapo kufikia mwaka 2020 Watumishi 45 watakuwa wamenufaika na mafunzo hayo kutoka Utawala, kada za Ulinzi na Usalama, Tehama, na Uendeshaji.
Msimamizi Mwandamizi na Mkaguzi wa Usalama wa anga Sanghoom (Mark) Lim
akitoa mafunzo kwa Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, Uendeshaji na uzuiaji
wanyamapori kuhusu masuala ya Usalama katika Viwanja vya Ndege ndani ya
Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
cha Julius Nyerere (JNIA TB II).
Watendaji
wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka Menejimenti na
Vitengo vya Usalama, Uendeshaji na uzuiaji wanyamapori wakiwa katika
mafunzo ndani ya Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP) katika Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA TB II).Walioketi mbele kushoto
ni Meneja Rasilimali watu na Utawala Bw. Abdi Mkwizu kulia ni Mkurugenzi
wa kituo cha Mafunzo ya Anga cha Kiwanja cha Ndege cha Incheon Bw. Chin
Hyong, Ryu.
Meneja
wa Mafunzo kutoka Kiwanja cha Ndege cha Incheoni Bi. Ji-Yoon Park
akitoa mafunzo kwa Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, Uendeshaji na uzuiaji
wanyamapori kuhusu namna ya kuandaa mpango wa kuwaongezea uwezo
watendaji katika Viwanja vya Ndege. Mafunzo hayo yamefanyika ndani ya
Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
cha Julius Nyerere (JNIA TB).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...