Mmoja wa wakulima wa tumbaku katika kijiji cha kasokola akichambua zao hilo
Baadhi ya wakulima wa kasokola wakisiliza elimu ya Bima ya Afya kutoka kwa wataalamu wa mfuko huo
Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Juma Michael akitoa elimu juu ya mpango wa ushirika afya kwa wakulima wa chama cha ushirika kasokola
Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Katavi Luhigiza Sesemkwa akizungumza na wakulima katika kijiji cha Kasokola

……………………………..


Na Ripota Wetu… Katavi


Wakulima wa zao la tumbaku katika kijiji cha Kasokola katika halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wameishukuru serikali kwa kuwaanzishia mpango wa Ushirika Afya; unaosimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya; utakaowawezesha kupata matibabu kwa urahisi bila malipo kwa kipindi cha mwaka mzima; na hivyo kuwezesha familia zao kupata matibabu na kuondokana na adha ya kutegemea dawa za kienyeji pindi wanapougua kutokana na kukosa fedha za matibabu

wakulima hao wametoa shukurani hizo katika mkutano mkuu wa sita wa chama cha msingi cha ushirika cha kasokola ambapo walisema mpango huo utaondoa adha ya kushindwa kutibiwa kwa kukosa fedha hasa katika msimu ambao sio wa mavuno

Bwana Hussein Mobi ni mmoja wa wakulima wa tumbaku katika kijiji hicho, alisema mwaka uliopita alitakiwa kufanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa tumbo na alitumia gharama kubwa lakini ujio wa mpango huo utakuwa mkombozi kwa wakulima walio wengi

Aidha wakulima hao walikitaka chama hicho kuandaa utaratibu wa kuwakata fedha kidogo kidogo kwa ajili ya kuchangia mfuko wa bima ya afya

Akizungumzia mpango huo uliozinduliwa rasmi na waziri mkuu mheshimiwa Kassim Majaliwa Julai mwaka jana; Mrajis Msaidizi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Katavi bwana Luhigiza Sesemkwa amesema serikali imeona iko haja ya kuwajumuisha wakulima katika fao la matibabu

Naye afisa masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya bwana Juma Michael alitaja baadhi ya faida za mfuko huo kuwa ni pamoja na kuwa na hakika ya kupata matibabu wakati wowote kwa zaidi ya vituo 7000 vya afya hapa nchini na hospitali mbalimbali

Aliongeza kuwa kwa sasa shirika linafanya zoezi la kutoa hamasa kwa wakulima katika maeneo mbalimbali nchi nzima ili wapate kuelewa umuhimu wa mfuko huo na kujiunga nao

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Katavi Bwana Said Juma alisema wakulima wa mazao matano ya kimkakati ikiwemo pamba, kahawa, korosho, chai na tumbaku wanahusishwa na mpango huo kuipitia vyama vya ushirika

Ametoa wito kwa wakulima kujiunga na mfuko ili kuondoa mashaka ya kupata matibabu pale wanapougua wakati familia hazina fedha hasa ukizingatia kuwa wakulima wanapata fedha kwa msimu wa mauzo ya mazao yao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...