WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali na Watanzania wote wataendelea
kumuenzi shujaa wao, Marehemu Edward Moringe Sokoine.
Amesema Marehemu Sokoine wakati wa uhai wake alijitoa kuchapa kazi kwa bidii na amelitumikia Taifa kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Aprili 6, 2019) katika mbio za marathon kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Sokoine. Mbio hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Waziri Mkuu amesema Serikali iliamua kwa makusudi kukiita Chuo Kikuu cha Kilimo jina la Sokoine ili kumuenzi shujaa huyo.Amesema Taifana Watanzania kwa ujumla wataendelea kufuata nyayo za Marehemu Sokoine katika mema mengi aliyolitendea Taifa la Tanzania na siku zote watandelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu.
Waziri Mkuu amesema kufanyika mbio hizo za Marathon ni ushahidi kwamba Marehemu Sokoine bado anakumbukwa na kuheshimiwa na Watanzania kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika ustawi wa Taifa.
Alisema katika uhai wake, Marehemu Sokoine alikuwa ni mfano bora wa kiongozi wa juu wa nchi aliyedhamiria kwa dhati kupambana na vitendo vya rushwa, uonevu, ubadhirifu na ufisadi.
“Leo hii tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Sokoine sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Magufuli inayoendeleza kwa vitendo utendaji, uandilifu na mtazamo aliokuwa nao marehemu Sokoine.”
Akizungumza kwa niaba ya familia ya Marehemu Sokoine, mtoto wa Marehemu, Namelok Sokoine alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kuwaenzi kwa vitendo waasisi wa Taifa la Tanzania.Alisema anafarijika kuona kwamba yale yote aliyoyaamini na kuyasimamia Marehemu Sokoine hivi sasa yanatekelezwa kwa kasi zaidi na ufanisi wa hali ya juu na Serikali inayoongozwa Rais Dkt. Magufuli.
Amesisitiza kwamba familia ya Marehemu Sokoine inaunga mkono kwa dhati juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na inaamini kwamba Tanzania yenye neema inakuja.Katika Marathon hiyo, washindi kwa uapnde wa wanaume waliokimbia kilomita 21 ni Joseph Panga, mshindi wa kwanza, na wa pili alikuwa ni Aliphonce Felix Simbu na mshindi wa tatu alikuwa Lazaro Damasi.
Upande wa wanawake kilomita 21, mshindi wa kwanza alikuwa ni Faulina Abdi Matanga, mshindi wa pili alikuwa ni Magdalena Shauri na mshindi wa tatu alikuwa ni Nathalia Elisante.Waliohudhuria katika mashindano hayo ni pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Wabunge na viongizi pamoja na wengine wa Serikali.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,JUMAMOSI, APRILI 6, 2019

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuzungumza katika
Marathon ya Kumbukumbi ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe
Sokoine iliyofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
Aprili 6, 2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mtoto wa Marehemu Edward Sokoine, Namelok Sokoine akitoa salamu za
familia katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu
Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha,
Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Marathon ya Kumbukumbu
ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja
wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Baadhi ya viongozi na wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa wakati alipozungumza katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35
ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri
Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wasanii wakimsikiliza
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakti alipoozungumza katika Marathoni ya
Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine
kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Joseph Panga zawadi ya shilingi
milioni moja ambaye aliibukuka kuwa Mshindi wa kwanza wa Marathoni ya
Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Edward Moringe Sokoine, Kilomita 21
wanaume kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6,
2019. Wa tatu kulia ni mshindi wa pili Alphonce Felix Simbu na Kulia ni
mshindi wa tatuLazaro Damas. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu na Rais wa Shirikisho la Riadha nchini, Anthony Mtaka, Mjane wa
Marehemu Edwad Moringe Sokoine, Napono Sokoine na wa tatu kushoto ni
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...