Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
TAKRIBANI watu 41 wamefariki dunia kufuatia ajali ya ndege ya Aeroflot Sukhoi Superjet ya nchini Urusi baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kushika moto na kulazimika kutua kwa dharura mjini Moscow hapo jana, shirika la utangazaji la Al jazeera limeripoti.

Video zimeonesha  ndege hiyo ya Sukhoi Superet -100 ilipata hitilafu na kulazimika kutua kwa dharura huku sehemu za ndege hiyo ikiwaka moto katika uwanja wa ndege  wa Sheremetyevo Moscow.

Baadhi ya picha za video zimeonesha baadhi ya abiria wakiruka kutoka katika sehemu zilizokuwa zinawaka na kuruka katika nyasi na sehemu salama.

Imeelezwa kuwa watoto wawili ni moja kati ya watu waliopoteza maisha na tayari wapelelezi kutoka Urusi wameshaanza kufanya uchunguzi kufuatia tukio hilo.

Waziri wa Afya wa Moscow Dmitry Matveyev amesema kuwa katika ajali hiyo watu 11 wamejeruhiwa, na watatu kati yao wameruhusiwa kutoka hospitali na hali zao zinaendelea vizuri.

Mamlaka ya uwanja wa ndege Moscow Urusi umesema kuwa ndege hiyo ilitua kwa dharura baada ya tatizo la kiufundi kutokea ikiwa angani na  wachunguzi watafanya utafiti kupitia mashahidi, wahanga pamoja na wafanyakazi wa ndege wa la shirika hilo.

Ndege hiyo ya Sukhoi  aircraft ilikuwa inaruka kutoka Moscow kuelekea mji wa kaskazini wa Urusi (Murmansk) kabla ya kurudi uwanjani na ilibeba abiria 73 na wafanyakazi wa ndege 4.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...