Said Mwishehe,Globu ya jamii


WATU 14 wameugua kipindupindu na mmoja kati yao amefariki dunia kwa ugonjwa huo katika Halmashauri ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia kuibuka kwa ugonjwa huo, Kaimu Meya wa Halmashauri ya Ilala Omar Kumbilamoto amesema baadhi ya wagonjwa wametoka maeneo ya Buguruni.

"Kipindupindu kimeingia kwenye manispaa yetu kwani tayari kuna watu 14 wameugua ugonjwa huo na mmoja kati yao amefariki dunia, wengine wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa na watu wanne bado wanaendelea kubapata matibabu,"amesema Kumbilamboto.

Amefafanua sababu za kuibuka kwa ugonjwa huo unatokana na mvua ambazo zimenyesha siku za karibuni na kibaya zaidi kuna baadhi ya watu waliokuwa wanafungulia maji machafu kwenye maji ya mvua, hivyo kusababisha kipindupindu.

Kumbilamoto amesema kutokana na kuibuka kwa ugonjwa huo wamechukua tahadhari ili usiendelee huku manispaa hiyo ikiweka mikakati ya kukomesha ugonjwa huo.

Pia amesema wananchi wanapaswa kubadili tabia kwa kutochafua mazingira kwani magonjwa mengi ya mlipuko chanzo chake ni uchafu.

Wakati huo huo Kaimu Meya huyo amesema Halmshauri ya Ilala tayari imeshatoa Sh.milioni 52 kwa ajili ya kununua dawa za kutibu ugonjwa wa Dungeu.

"Halmashauri ya Ilala imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa Dengue,"amesema Kumbilamoto na kuongeza fedha nyingi zinatumika kwa ajili ya kuhakikisha afya za wananchi zanakuwa salama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...