Na Heri Shaban,Dodoma
MWENYEKITI wa Taasisi ya Utalii 255 ambaye pia ni Mbunge wa Mkoa wa kaskazini Unguja Angelina Malembeka ,amewahamasisha Watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za Mbunga za Utalii, zilizopo nchini ili kujifunza utalii wa ndani na kuona vivutio vilivyopo.
Mbunge Malembeka aliyasema hayo Bungeni Dodoma leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada kupokea wageni wake ,Wahamasishaji wa Kundi la Utalii 255 kutoka Tanzania Bara leo walishiriki kusikiliza kikao cha maswali na majibu Bungeni Dodoma.
Alisema ziara ya Wahamasishaji wa Utalii wa 255 Kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar wapo katika ziara ya siku tatu ,wameanza kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kesho Mei 4 ziara inaelekea kutembelea Mbuga ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangile Mkoa wa Mnyara.
"Hii ni sehemu ya kampeni ya kutangaza Utalii wa ndani ,kundi la Utalii 255 linawataka Watanzania kuweka mazoea ya kutembelea hifadhi za Taifa kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo wanyama kama sehemu ya kujifunza"alisema Malembeka
Alisema Utalii 255 ilianzishwa hivi karibuni,ikiwa na lengo la kuwahamasisha na kuwakumbusha Watanzania kuweza kujiwekea utaratibu wa kutembelea Hifadhi na Vivutio vya Utalii vilivyopo Nchini, Ziara hii imewashirikishaka Vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...