Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akikabidhi fedha kiasi cha Shilingi milioni moja kwa Wabunge mashabiki wa Timu ya Soka ya Yanga iliyopokelewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mheshimiwa Anthony Mavunde, Ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma. Fedha hizo ni kwa ajili ya kuichangia Timu ya Yanga.
Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi fedha kiasi cha Shilingi milioni moja kwa Wabunge mashabiki wa Timu ya Soka ya Yanga kwa ajili ya kuichangia timu hiyo, Ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma .
(PICHA NAOFISI YA BUNGE)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...