VIONGOZI wa nchi za Kiarabu wameishutumu Iran
na kuitaka kuacha kuingilia mahusiano ya nchi
nyingine.
Kwa mujibu wa Mtandao wa DW umesema kuwa
shutuma hizo nchi hizo wamezitoa wakati
wakihitimisha mikutano miwili ya kilele ya dharura
nchini Saudi Arabia baada ya mashambulizi kwenye
ukanda wa Ghuba. Iran ililaumiwa kwa
mashambulizi hayo.
Taarifa ya kuhitimisha mikutano hiyo imechapishwa
mapema leo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za
kiarabu, Arab League, Ahmed Aboul Gheit baada ya
mkutano wa jumuia hiyo.
Mikutano ya jumuia hiyo pamoja na Baraza la
ushirikiano wa mataifa ya Kiarabu, GCC katika Mji
wa Mecca iliitishwa baada ya mashambulizi kwenye
meli nne za mafuta katika Pwani ya Umoja wa
Falme za Kiarabu, UAE na yale ya ndege zisizo na
rubani kwenye mabomba ya mafuta nchini Saudi
Arabia yaliyofanywa na waasi wa Houthi wa Yemen
wanaoungwa mkono na Iran.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...