Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umewahimiza Watanzania kutembelea Hifadhi ya msitu wa asili wa Magamba uliopo wilayani Lushoto mkoani Tanga ili kushuhudia vivutio vya utalii vilivyomo.

Imesisitiza katika hifahi ya msitu wa Magamba atakayekweda atashuhudia kila aina ya utalii kwani wamejaaliwa kuwa na vivutio vingi ambavyo vingine havipatikani kokote zaidi ya kwao ukiwemo Mlima wenye pango la Mjerumani alilolitumia kujificha wakati wa mapigano ya vita ya kwanza ya Dunia.

Akizungumza wilayani Lushoto mkoani Tanga Mhifadhi Mkuu wa Msitu wa Magamba Gretuda Nganyagwa alisema kimsingi ndani ya hifadhi hiyo kuna kila aina ya kivuto cha utalii ambapo watakaofika hatachoka kuangalia.

Akizungumzia zaidi hifadhi hiyo yenye utalii wa asili , alisema imezungukwa vijiji 21 ambapo kati ya hivyo vijiji 17 vipo wilayani Lushoto na vijiji vinne vipo katika Wilaya ya Korogwe na kwamba hifadhi inayo mimea ya aina nyingi, wanyama wengi. 

"Pia inatumika kwa ajili ya mafunzo,kufanya tafiti mbalimbali na kubwa zaidi inatumika kwa ajili ya utalii Ikolojia na ndio maana tunatamani kuoana Watanzania wengi wanakuja kushuhudia kwa macho haya ambayo tunayaeleza,"amesema.

Alisisitiza ndani ya Magamba pia kuna vingonga wa pembe mbili, nyani aina ya mbega, kuna wadudu wadogo na wakubwa, wanyama wakubwa lakini ni vigumu kuwaona hadi uende katikati ya msitu, ndege na buibui.

Pia amesema kuna maporomoko ya maji ambayo yanatiriria kwa mpangilio unaovutia huku pia watakaofika watapata fursa ya kwenda kuona pango la Mjerumani ambalo lipo kwenye kilele cha mlima ambalo walilitumia kujificha enzi za vita ya kwanza ya dunia.

"Magamba ni hifadhi inayotambulika kisheria tangu enzi za Ukoloni, ina mipaka imara na ndio maana inatambulika kama hifadhi ya Serikali ambayo TFS tumepewa jukumu la kuisimamia.Kadri siku zinavyokwenda idadi ya watalii wa ndani inaongezeka na hivyo kuchangia katika kuongeza pato la nchi yetu,"alisema Nganyagwa.

Aliongeza TFS wanaendelea kutoa hamasa kwa Watanzania kutenga muda ili wafike Magamba kwani ni eneo zuri la kwenda hata na familia kwa kuwa kuna huduma za makambi, kuna maua na watakaokwenda watapata nafasi ya kuimarisha viungo kutokana na kutembea ndani ya hifadhi.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Mawasiliano wa TFS Tulizo Kilaga amesema kwa sasa wapo katika kampeni ya kuhamasisha Watanzania kujenga tabia ya kutembelea hifadhi za misitu ya asili ambako kuna vivutio vya utalii wa asili.

"TFS tunasimamia hifadhi za misitu ya asili 17 nchini, na hifadhi hizo ziko katika maeneo mbalimbali na kote huko watakaokwenda wataona namna ambavyo Mungu ameipendelea nchi yetu kwa kuweka kila aina ya kivutio cha utalii.Hivyo nitoe rai kwa Watanzania ni wakati wenu kutembelea vivutio vyetu vya utalii,"amesema Kilaga.

Alifafanua kwa sasa wanakwenda katika msimu wa utalii na hivyo TFS imejipanga kuhakikisha wananchi wenye utayari wa kutembelea hifadhi za misitu ya asili wanapata nafasi hiyo na kuona kila ambacho watatamani kukiona na hasa utalii wa asili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...