Mkuu
wa mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge, akikata utepe kuzindua ofisi
mpya za kanda ya kati na duka la kisasa la Vodacom Tanzania Plc jijini
Dodoma. Kampuni hiyo imezindua makao yake makuu ya Kanda ya Kati ikiwa
ni kuunga mkono juhudi za Serikali kuhamishia shughuli zake mji mkuu
kwa kuhakikisha wanapata mawasiliano imara na huduma sanifu. Wa pili
kulia ni Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, Anthony Mavunde na Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Kati wa kampuni
ya Vodacom Tanzania, Bi Grace Chambua. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha
Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu na Kaimu
Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Linda Riwa.
Mkuu
wa mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge akizungumza katika uzinduzi wa
ofisi mpya za Kanda ya kati na duka la kisasa la Vodacom Tanzania Plc
jijini Dodoma. Kampuni hiyo imeunga mkono jitihada za serikali ya awamu
ya tano kuhamishia shughuli zake mji mkuu kwa kuhakikisha wanapata
mawasiliano imara na huduma sanifu.
Naibu
Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony
Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa ofisi mpya na duka la kisasa la
Vodacom Tanzania jana jijini Dodoma. Kampuni hiyo imeunga mkono jitihada
za serikali ya awamu ya tano kuhamishia shughuli zake mji mkuu
kwa kuhakikisha wanapata mawasiliano imara na huduma sanifu.
Kaimu
Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa akizungumza
katika uzinduzi wa ofisi mpya na duka la kisasa la Vodacom Tanzania jana
jijini Dodoma. Kampuni hiyo imeunga mkono jitihada za serikali ya awamu
ya tano kuhamishia shughuli zake mji mkuu kwa kuhakikisha wanapata
mawasiliano imara na huduma sanifu.
Mkuu
wa Mauzo wa Kanda ya Kati wa Vodacom Tanzania, Bi Grace
Chambua akizungumza katika uzinduzi wa ofisi mpya na duka la kisasa la
Vodacom Tanzania jana jijini Dodoma. Kampuni hiyo imeunga mkono jitihada
za serikali ya awamu ya tano kuhamishia shughuli zake mji mkuu
kwa kuhakikisha wanapata mawasiliano imara na huduma sanifu. Walio keti
ni Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony
Mavunde (wa kwanza kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge
(kati) na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...