Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katikati akikata utepe kufungua soko la kuuzia Dhahabu na madini ya vito wilaya ya Tunduru kama utekelezaji wa agiza ka Rais Dkt John Magufuri aliloagiza kila wilaya na mkoa ambao una madini kufungua soko la kuuzia madini ambalo litawezesha wauzaji na wanunuzi kuuzia madini. Picha na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katikati akipiga makofi jana mara baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa soko la kuuzia Dhahabu na madini ya vito katika wilaya ya Tunduru mkoani humo,wa kwanza kushoto  mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Mkwanda Sudi ,Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo na kulia Afisa madini Mkazi wa wilaya hiyo Juma Kapela.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme akiongea na baadhi ya wanunuzi wa Madini  waliosimama kushoto wakati wakati wa Ufunguzi wa soko la kuuzia Dhahabu na madini ya vito wilayani Tunduru,kulia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Tunduru ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme amesema, kiasi cha shilingi milioni 44,950,910 zimepkusanywa katika kipindi cha wiki moja kutoka tarehe 6 hadi 9 Mwezi huu kutokana na kodi na tozo mbalimbali za madini tangu Serikali ilipoanzisha maduka ya kuuzia na kununua madini mkoani Ruvuma.

Mkuu wa mkoa ametoa kauli hiyo jana, wakati akifungua soko la kuuzia Dhahabu na madini ya vito wilayani Tunduru ambapo alisema, kati ya fedha hizo shilingi ml 9,916, 254 zimetokana na mrabaha na shilingi ml 2.5 ni ushuru.

Mkuu wa mkoa alisema,tangu Serikali ilipoweka sheria ya kuanzishwa kwa soko la madini kumekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kuongezeka kwa mapato ya Serikali na udhibiti wa madini ambayo kabla ya sheria hiyo kulikuwa na vitendo vingi vya utoroshaji madini na ukwepaji mkubwa wa kodi.

Alisema, katika kipindi hicho jumla ya gram 2824.2 zimepatikana kati ya hizo gram 2540 madini ya vito na dhahabu iliyopatikana ni gram 364.2.

Aidha Mndeme,ameagiza kufanyiwa ukaguzi wa mizani na vifaa vingine vya kupima madini hasa baada ya kubaini kuwa,baadhi vipimo vinavyotumika haviko sahihi jambo linaloweza kusababisha udanganyifu na hivyo kuikosesha Serikali taarifa mapato halisi.

Alisema, lengo ni kufahamu thamani ya madini yetu kwani kwa muda mrefu kumekuwa na udanganyifu mkubwa unaofanywa na wafanya biashara wa madini.

Alisema, ufunguzi wa soko la madini katika wilaya ya Tunduru na Songea mkoani humo ni utekelezaji wa Agizo la Rais Dkt John Magufuri ambalo linalenga kupata uhakika wa takwimu za madini,soko na uhakika wa bei na kuondoa unyanyasaji kwa wachimbaji wadogo unaofanywa na wanunuzi.

Amewataka wananchi na wachimbaji wadogo wa madini katika mkoa huo kuwa walinzi wazuri wa rasiimali zetu za madini na kusisitiza kuwa yeyote atakayekamatwa anatorosha madini atachukulia hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani sambamba na kufutiwa leseni.

Hali kadhalika mkuu wa mkoa, ameziomba taasisi za fedha ikiwemo Benki kufungua huduma za fedha katika eneo la kuuzia madini ili kuwaondolea usumbufu wanunuzi na wauzaji madini kufuata fedha mbali sambamba na kuwataka wachimbaji wadogo kuhakikisha wanafungua Akaunti badala ya kutembea na fedha nyingi mifukoni jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.

Awali Afisa Madini mkazi wa wilaya ya Tunduru Juma Kapela alisema, wilaya ya Tunduru imebarikiwa kuwa na madini mbalimbali ya thamani kama Dhahabu,madini ya vito na shaba.

Kapela alisema, Ofisi ya Afisa madini mkazi inasimamia jumla ya leseni hai 342 za uchimbaji mdogo na imeshapokea maombi mapya yaliyopokelewa ni 56 ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini ambayo yapo katika hatua za kupitiwa kama yanakidhi vigezo ili yaweze kutolewa leseni.

Alisema, hadi sasa jumla ya leseni 239 zimepewa hati za makossa na leseni 1,342 zimefutwa kwa kutotimiza masharti ya umiliki wa leseni hizo kwa mujibu wa sheria.Alisema, kufunguliwa kwa Soko la madini katika wilaya ya Tunduru kutafungua milango kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini walioko katika wilaya ya Tunduru na maeneo jirani kupata sehemu ya kuuzia na kununua madini.

Kwa upande wao wachimbaji wadogo wa madini ,wamempongeza Rais Dkt John Magufuri kwa kukubali kukutana na wadau wa sekta ya madini ili kusikiliza kero za sekta ya madini.

Hata hivyo,wameiomba Serikali iweze kutengeneza mazingira mazuri ya soko la ununuzi wa madini ya vito kwa sababu wanunuzi hao wapo katika Kampuni tofauti hivyo kukaa chumba kimoja Zaidi ya mnunuzi mmoja inaondoa usiri wa Kampuni kwa Kampuni na mchimbaji anayehitaji kuiuzia.

Makamu mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wadogo wa Madini Mohamed Mlangwa alisema, hali hiyo inatokana na ukweli kwamba madini ya vito hayana bei maalum kama ilivyo kwa Dhahabu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...