Na Shamimu Nyaki- WHUSM
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa Serikali inatambua mchango na jitihada kubwa zinazofanywa na Machifu wa makabila mbalimbali ya Tanzania katika kuhifadhi,kulinda na kuendeleza Mila na Desturi za Taifa hili.
Mhe.Shonza ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati alipofanya Kikao na Machifu wa Mkoa wa Singida pamoja na Rorya waliofika ofisini kwake kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Sekta ya Utamaduni ambapo amewaeleza kuwa wao kama viongozi wenye dhamana ya kuendeleza mila na desturi za makabila yao ni jukumu lao kuhakikisha kuwa wanafanya kazi hiyo kwa lengo la kuutangaza Utamaduni wa nchi yetu.
"Serikali inatambua juhudi mnazofanya katika kuendeleza Mila na Desturi za maeneo yenu ndio maana imetenga maeneo ambayo mnakutana kufanya shughuli za kiutamaduni ikiwemo kuandaa mfumo rasmi wa kuwatambua"alisema Mhe.Shonza.
Aidha amewataka machifu hao kushirikiana na Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri wakati wanapotaka kufanya shughuli za kiutamaduni katika maeneo yao.
Kwa upande wake Chifu wa Rorya Bw.Ngoja Ongabo ameishauri Serikali kutoa ushirikiano kwa Machifu katika Wazo lao la kuanzisha Baraza la Wazee ambalo litasaidia kuwaunganisha Wazee wa makabila mbalimbali yaliyopo hapa nchini na kujadili namna bora ya kuhifadhi mila na Desturi zetu.
Naye Chifu Omary Hamis wa Singida ameiomba Serikali kuweka mipaka katika maeneo ya kufanyia shughuli za utamaduni ili kuepuka migogoro ya ardhi inayotokana na wanachi kuvamia maeneo hayo.
Hata hivyo Serikali imepokea ushauri uliotolewa na machifu hao ambapo imeahidi kuzifanyia kazi.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza(kulia)
akizungumza na Machifu kutoka Mkoa wa Singida na Mara Wilaya ya Rorya
ambao walimtembelea ofisini kwake Mei 28 Jijini Dodoma kujadili masuala
mbalimbali yanayohusu namna ya kuendeleza na kuhifadhi Mila na Desturi
za nchi yetu.
Mkurugenzi
Idara ya Mendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na
Michezo Dkt. Emmanuel Temu akizungumza katika kikao cha Naibu Waziri
Mhe Juliana Shonza (wa pili kulia) pamoja na Machifu wa Singida na Rorya
kilichokua na lengo la kujadili namna ya kuendeleza na kuhifadhi Mila
na Desturi za nchi yetu kilichofanyika Mei 28,Jijini Dodoma.
Chifu
Ngoja Ongabo wa Rorya (katikati) akieleza jambo katika kikao cha Naibu
Waziri Mhe Juliana Shonza (hayupo katika picha) pamoja na Machifu wa
Singida na Rorya kilichokua na lengo la kujadili namna ya kuendeleza na
kuhifadhi Mila na Desturi za nchi yetu kilichofanyika Mei 28,Jijini
Dodoma.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza(kulia)
akisikiliza na kuandika mchango wa Bw.Iddi Juma Ndabu kutoka Singida
wakati alipofanya kikao na Machifu kutoka Mkoa wa Singida na Mara Wilaya
ya Rorya ambao walimtembelea ofisini kwake Mei 28 Jijini Dodoma
kujadili masuala mbalimbali yanayohusu namna ya kuendeleza na kuhifadhi
Mila na Desturi za nchi yetu.
Chifu
Omary Hamis wa Singida (kulia) akieleza jambo katika kikao cha Naibu
Waziri Mhe Juliana Shonza (hayupo katika picha) pamoja na Machifu wa
Singida na Rorya kilichokua na lengo la kujadili namna ya kuendeleza na
kuhifadhi Mila na Desturi za nchi yetu kilichofanyika Mei 28,Jijini
Dodoma.Kushoto ni Bw.Iddi Juma Ndabu kutoka Singida.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...