Timu ya Viongozi Watendaji Wakuu wa Wilaya ya Kati ikiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar inakamilisha uchunguzi wa kuwabaini Watu waliohusika na uvamizi wa Shamba la Marehemu Binti Kangeta ambae amefariki Dunia akiwa hana mrithi.

Wakati Shamba hilo liliopo Shehia ya Ghana Wilaya ya Kati kwa sasa linatumiwa na Wananchi wa maeneo hayo kwa shughuli za Kilimo wakijitokeza Watu waliovamia Shamba hilo kinyume na Sheria na Taratibu za Serikali wakiwaonya Wananchi hao kuondoka katika maeneo hayo wakidai wameshamilikishwa Shamba hilo kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Mkuu wa Wilaya ya Kati Bibi Hamida Mussa Khamis aliwaeleza Wananchi wa Maeneo hayo kwamba sheria za Ardhi zilizopo Nchini ziko wazi zikielezea kwamba mmiliki wa shamba lolote akiwa hana mrithi anapofariki Dunia umiliki wake hurejea Serikalini.

Bibi Hamida aliweka wazi kwamba kwa sasa Shamba hilo licha ya kwamba Wananchi hao wanaendelea na shughuli zao za Kilimo lakini umiliki wake uko chini ya Serikali Kuu.

Alionya kwamba Serikali haitasita kumchukulia hatua za Kisheria Mtu au Kikundi chochote chenye nia ya kutaka kujimilikisha Shamba hilo kinyume na Taratibu jambo ambalo likiachiliwa kuendelea linaweza kuleta mgogoro unaoweza kuepukwa mapema.

Bibi Hamida alifahamisha kwamba Mtu yoyote anayetaka kutumia shamba hilo hawezi kujimilikisha mwenye binafsi bali anawajibika kufuata Taratibu kwa kuandika maombi na kupelekea Serikalini yatakayofikia hatua ya kupata ithibati kamili juu ya matumizi ya Shamba hilo.

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mohamed alionya kwamba Wizara haitosika kumsimamisha Kazi na hatimae kumfukuza Kazi mara moja Mfanyakazi ye yote atakayebainika kujihusika na migogoro ya Ardhi.

Nd. Shaaban Seif aliwathibitishia Wananchi hao kwamba hakuna Kiongozi ye yote wa Ofisi hiyo inayosimamia shughuli za Serikali anayeweza kutoa kibali au ruhusa ya Matumizi ya Shamba au Ardhi wakati Wizara inayosimamia jukumu hilo ipo kwa mujibu wa Sheria na Taratibu za Nchi.

Katibu Mkuu Shaaban alimtahadharisha Sheha wa Shehia ya Ghana kuwa makini na baadhi ya Matapeli wenye tabia ya kuwatisha Wananchi Mitaani kwa visingizio vya kuwa wako karibu na Wakubwa wenye madaraka ya juu Serikalini.

Kwa upande Wao Wanachi wanaolima katika Shamba hilo wameelezea faraja yao kutokana na ujio wa Timu hiyo ya Viongozi Watendaji Wakuu wa Wilaya ya Kati ikiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kufuatilia tatizo hilo.

Walisema faraja yao imekuja kufuatia dalili ya kuzimwa kwa vitisho la Watu waliojifanya kupewa umiliki wa Shamba hilo ambao tayari walikuwa wameshaanza harakati za kuweka mipaka huku wakiwaonya Wananchi hao kuacha kulima mara moja ndani ya shamba hilo
 Timu ya Viongozi Watendaji Wakuu wa Wilaya ya Kati ikiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakiangalia Shamba la Marehemu Binti Kangeta ambae amefariki Dunia akiwa hana mrithi liliopo Kijiji cha Ghana Wilaya ya Kati.
 Baadhi ya Wakulima wa Kijiji cha Ghana wanaolima katika Shamba la Marehemu Binti Kangeta lililovamiwa na Watu wasiojuilikana na kuamuru Wakulima hao waache kulima mara moja.
 Mkuu wa Wilaya ya Kati Bibi Hamida Mussa Khamis akiwaeleza Wananchi wa Ghana sheria za Ardhi zilizopo Nchini ziko wazi zikielezea mmiliki wa shamba lolote akiwa hana mrithi anapofariki Dunia umiliki wake hurejea Serikalini.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mohamed akitoa onyo kwa kumsimamisha Kazi na hatimae kumfukuza Kazi mara moja Mfanyakazi ye yote atakayebainika kujihusika na migogoro ya Ardhi.
 Bibi Tatu Mohamed Seif akishukuru kwa niaba ya Wakulima wenzake ujio wa Timu ya Viongozi hao iliyoleta faraja kwao kujenga matumaini ya kuendelea kulima katika shamba la Marehemu Bibi Kangeta huko Ghana.

Baadhi ya maeneo ya Shamba la Marehemu Bibi Kangeta liliopo Kijiji cha Ghana Wilaya ya Kati lililovamiwa na Watu Matapeli wanaotaka Wakulima wa eneo hilo waondoke. Picha na – OMPR – ZNZ.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...