Na Ripota wa Michuzi TV 

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Hazina ya Magomeni wametia fora katika mashindano ya kitaaluma kwa shule za msingi katika Jiji la Dar es Salaam. 

Mashindano hayo ya kitaaluma yameandaliwa na Shule za Feza kwa kushirikisha shule mbalimbali za msingi za umma na za binafsi jijini Dar es Salaam. 

Mkuu wa Taaluma wa shule ya Hazina Dennis Nyakerandi amesema mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza kwenye mashindano hayo Salma Sadiki Mushi ametoka katika shule yao. 

Amewataja wanafunzi wengine wa Hazina walioingia 10 bora kwenye mashindano hayo ni Ibrahim Sharif aliyeshika nafasi ya pili na nafasi ya nne ilichukuliwa na Patricia Benatus wa shule hiyo. 

Wengine ni Sahill Imam aliyeshika nafasi ya nne, Maliki Yassin nafasi ya sita na nafasi ya nane kwenye mashindano hayo ilichukuliwa na Khaulat Majid wa shule hiyo ya Hazina. Hivyo amesema matokeo hayo yamewapa motisha kuwa wanaendelea kufanya viziuri kwenye taaluma na wanatarajia kufanya vizuri zaidi kwenye mitihani inayokuja. 

Ameongeza ushindi huo haukuja tu bali umetokana na jitihada za walimu kuwaandaa wanafunzi kwaajili ya mitihani. "Hivyo sisi imetupa moyo kazi tunayofanya inazaa matunda." 

Pia amesema kwenye mashindano hayo wanafunzi wamefanya mtihani wa Hisabati na Sayansi ambapo wanafunzi walipaswa kumaliza ndani ya saa mbili na kwamba wao walipeleka wanafunzi 10 na sita wakaingia 10 bora tena kwenye nafasi za kwanza. 

"Tunajivunia mafanikio haya kwani wanafunzi walikuwa wengi sana lakini wamefanya vizuri.Tunawapongeza walimu wetu kwa mafanikio haya,"amesema na kusisitiza wataendelea kufanya vizuri siku hadi siku. 
Mkuu wa Taaluma wa Shule ya Msingi Hazina, Dennis Nyakerandi akimpa zawadi ya vitabu mwanafunzi wa shule hiyo, Salma Mushi kwa kuwa wa kwanza kwenye mashindano ya Hisabati na Sayansi yaliyoshirikisha zaidi ya wanafunzi 350, yaliyoandaliwa na shule za Feza jijini Dar es Salaam. Wengine nyuma ni wanafunzi wa shule hiyo waliofanikiwa kuingia 10 bora kwenye mashindano hayo. 
Wanafunzi wa shule ya Msingi Hazina ya jijini Dar es Slaam, wakiwa na vyeti vyao walivyokabidhiwa baada ya kushinda na kuingia 10 bora kwenye mashindano ya Hisabati na Sayansi shindano lililowashirikisha zaidi ya wanafunzi 350 kutoka shule mbalimbali. Shindano hilo limefanyika katika shule ya Feza. Wanafunzi wengine wa shule hiyo wanaoshuhudia nao walifanikiwa kuingia 10 bora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...