Na Editha Edward- Michuzi TV,Tabora

Kamati ya Ulinzi na usalama kupitia jeshi la polisi mkoa wa Tabora limeahidi Kuongeza nguvu ya Ulinzi na usalama katika Soko kuu la Madini mkoa wa Tabora kwa kutumia mbinu za kiteknolojia na kuimarisha Ushirikiano dhidi ya Wachimbaji wadogo na Serikali lengo ikiwa ni kuhakikisha wauzaji na wanunuzi wa Madini wote wanakuwa na Ulinzi na usalama dhidi ya biashara hiyo

Yamesemwa hayo hii leo mjini Nzega Mkoani Tabora katika Ufunguzi wa soko la Madini ambalo limejengwa kisasa huku likizingatia Weledi wa juu pamoja na kutekeleza agizo la Serikali ya Awamu ya Tano

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Kamishina Msaidizi Mwandamizi Emmanuel Nley amesema biashara hiyo itakuwa safi na salama Kamati ya Ulinzi imejipanga kuimarisha suala hilo kwa vitendo zaidi

"Soko kuu la kununua na kuuza dhahabu litaimarishwa sana kutakuwa na Askari wa aina mbili Askari wanaovaa Uniform watakuwa hapa na Askari wanaovaa kiraia watakuwa hapa katika jengo hili na zitafungwa teknolojia zilizoimatishwa kutakuwa na CCTV Camera na vyombo vya moto kwa hiyo katika jengo hili kutakuwa na Usalama "Amesema Nley

Kwa upande wake katibu Tawala mkoa wa Tabora Robert Makungu amesema soko hilo limezingatia vigezo vya kibiashara kwani huduma za kifedha zinapatika bila usumbufu wowote

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema hatarajii kusikia watu wanatorosha Madini ."Sitaki kusikia mtu anakamatwa kwa kosa la kutorosha Madini atakayekamatwa atachukuliwa hatua za sheria na mtu huyo atakayefanya hivyo ujue hataki maendeleo ya nchi "Amesema Mwanri

Aidha Serikali ya mkoa wa Tabora imeendelea kuwatoa hofu wauzaji na Wafanyabiashara wa kuwauzia Madini katika soko hilo ambapo imesema bei itakuwa ni rafiki na hakutakuwa na ubabaishaji na soko hilo litawasaidia Wafanyabiashara wa Madini kutokwenda nje ya mkoa kuuza madini yao kwani soko hilo limekidhi kila kitu.
Pichani ni Soko kuu la madini la  Mkoani Tabora lililopo Mjini Nzega  Tabor.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...