Na Mwandishi Wetu
WACHEZAJI  karate wa Tanzania, Mikidadi Kilindo na Elisiana Katani wameibuka washindi wa mashindano ya kata kwa upande wa wanaume na wanawake katika mashindano ya Afrika ya Mashariki na Kati yaliyomalizika jijini Kampala, nchini Uganda hivi karibuni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la JKA Tanzania, Fedeliko Nestory amewasifu wachezaji hao kwa kushinda medal hizo, sio kwa wao binafsi, bali kwa nchi pia.


Kilindo, mwenye dani 4 ( maarufu Ganchan) ambaye pia ni Mkufunzi Mkuu msaidizi wa JKA/Tanzania, ameshinda medali ya dhahabu, baada ya kuwashinda washiriki wengine kutoka nchi zaidi ya 10 zilizoshiriki katika upande wa kata (kuonyesha maarifa ya kupigana) kwa upande wa wanaume. Hii ni mara ya tano kwa Ganchan kushinda taji hili.

Pia ni mara ya kwanza kwa kushinda taji hili, akiwa miongoni mwa wanawake wachache wanaocheza mchezo huu hapa nchini.

Katani, ambaye pia ni mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Utoaji taarifa kwa Umma wa JKA/World Federation-Tanzania, ameshinda medali ya fedha , baada ya kushinda nafasi ya pili katika upande wa wanawake.

“Tunashukuru Mungu tumeshinda medali, tunaomba wadau wasaidie kuukuza mchezo huu hapa nchini,” wamesema Kilindo na Katani kutokea Kampala, kupitia ukurasa wa Facebook wa JKA/WorldFederation-Tanzania. 

Nestory amesema wawakilishi hao wameipeperusha vema bendera ya Tanzania kimataifa, huku akiomba serikali, mashirika ya umma, makampuni na watu binafsi kusaidia katika ukuaji na ushiriki wa mchezo huo katika michuano ya kimataifa.




















“Tuna mashindano mengi katika kalenda yetu yam waka, hivyo tunaomba wadau watusaidie,”

Amesema kuanzia July 1-7, Tanzania itakuwa mwenyeji wa semina ya ya Gasshuku na Mashindano ya kimataifa ambapo nchi 15, ikiwemo Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Zimbabwe, Zambia, Malawi, Angola, Botswana, Madagascar, Zimbabwe, Jamhuri ya Kongo na Afrika ya Kusini zimethibitisha ushiriki.

Miongoni mwa michuano mikubwa ambayo JKA Tanzania inategemewa kushiriki ni michuano ya Olimpiki itakayofanyika mwakani mjini Tokyo, Japan, huku mchezo huo ukiwa miongoni mwa michezo shiriki kwa mara ya kwanza.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...