Na Fatma Kassim
WIZARA ya Afya imesema suala la kukabiliana na Majanga si la Wizara ya
Afya pekeake linahitaji mashirikiano na taasisi mbalimbali kwa lengo
la kukabiliana na majanga yanayoweza kutokea.
Akifungua mkutano wa wadau wa afya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Halima Maulid Salum amesema ushirikiano wa taasisi tofauti katika nchi
ndio njia pekee itakayowezesha kuondosha hali ya hatari.
Alifahamisha kwa sasa Zanzibar imejiweka tayari katika kukabilina na
hali ya majanga mbalimbali ikiwemo ya maradhi ya miripuko ambapo
katika maradhi ya kipindupindu wameweza kupigahatua kubwa ya
kuyaangamiza kutoka na ushirikiano uliopo baina ya taasisi mbalimbali
ikiwemo Halmashauri na Wilaya.
Amesema Wizara ya afya itahakikisha inashirikiana na wadau wote
ikiwemo washirika wa maendeleo wakiwemo Shirika la Afya Duniani WHO
katika kujiweka tayari na hali ya majanga ya maradhi ya miripiko
yatakapo tokea ili yasiweze kuleta athari nchini.
Amezitaka Tasisi zote husika kupanga mipango madhubuti itakayo saidia
kukabiliana na hali yoyote ya hatari, majanga sambamba na kuondosha
kabisa maradhi na kuepuka miripuko.
Nae Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani aliyopo Zanzibar Dk.
Andemichael Ghirmay amesema kutokana na majanga yanayongezeka Duniani
kote ni vyema kuwepo kituo cha kuratib matukio ya kiafya Wizara ya
Afya alishauri.
Ameiomba Wizara ya afya kwa kushirikiana na sekta mbalimbali Kuchukua
hatua za makusudi za kuanzisha vituo vya dharura sehemu tofauti
ambavyo vitatumika katika kukabiliana na majanga mbalimbali pindipo
yatatokea.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halima
Maulid akifungua warsha ya wadau wa kutathmini athari za matukio ya
Kiafya uliofanyika katika ukumbi wa Kitengo Shirikishi cha Afya ya
Uzazi na Watoto Kidongochekundu Mjini Zanzibar.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Ofisi ndogo
ya Zanzibar Dr. Andemichael Ghirmay akisoma hutuba yake katika
Mkutano wa wadau wa afya na kutoa pendekezo la kuwepo kituo cha
kuratib matukio ya kiafya Wizara ya Afya.
Dkt. Mlenge Mgendi akiwasilisha rasimu ya mwazo ya ripoti
ya wadau wa Afya ya kutathmini athari na matukio ya kiafya Zanzibar.
Baadhi ya wadau wa Mkutano wa kutathmini athari na
matukio ya kiafya Zanzibar wakifuatulia mkutano huo.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar
Halima Maulid (watano kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na wadau
wa afya kutoka taasisi mbalimbali.
Picha na Makame Mshenga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...