Na Woinde Shizza , Michuzi TV-Arusha
WAREMBO 23 wanaoshiriki kinyang'anyiro cha kumpata mrembo mmoja wa Mkoa Arusha wametoa elimu ya afya na usafi kwa wanafunzi wa kike wanaosoma katika Shule ya Msingi Naurei na Sekei .
Mbali na kutoa elimu hiyo yenye leng la kuwandaa wasichana ambao wanakaribia kuvunja ungo, pia warembo hao wametoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi ambao wamevunja ungo pamoja na kuwapa elimu ya kujinga na U.T.I.
Akizungumza na wanafunzi wa shule hizo mmoja wa warembo hao Anna Fanuel(23)amesema wameona kuna kila sababu ya kutoa elimu ka wanafunzi hao wakiwamo waliovunja ungo na wale ambao bado hawajavunja ungo kwani elimu hiyo wanastahili kuipata wote.
"Kwa sehemu kubwa elimu ambayo tumeitoa ni kumsaidia msichana aliyekuwa shuleni kutambua kuwa ni muhimu kuzingatia usafi muda wote.Wakiwa wasafi maana yake wanajiepusha na magonjwa ambayo msingi wake ni uchafu,"amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mashindano ya Miss kwa Mkoa wa Arusha Tilly Chizenga amesema wamegawa taulo za kike zaidi ya 1000 kwa wanafunzi wa shule hizo mbili na wana mpango wa kuendelea kuzigawa sambamba na utoaji elimu kwa shule nyingine za mkoani hapa.
Kuhusu warembo hao amesema watakaa kambini kwa muda wa mwezi mmoja na kisha wataingia katika kinyanganyiro cha kumpata mrembo mmoja.Mashindano hayo yatafanyika mwishoni mwa Juni mwaka huu.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewapongeza warembo hao kwa utoaji wa elimu na ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi hao.
Amesema Serikali ipo bega kwa bega kuhakikisha mrembo wa Arusha anapatikana, na si Arusha tu, bali wanatoa Miss Tanzania."Tunatamani hata Mrembo wa Dunia safari hii awe anatoka Arusha."
Amewaambia warembo hao wanatakiwa kufahamu kuwa urembo unaanzia kwenye tabia, muonekano na hata sura na kwamba Serikali ya Wilaya inafuatilia hatua kwa hatua mashindano hayo.
"Wenye tabia nzuri hao watafika mbali lakini mwenye tabia mbaya na ya hovyo ni vema wakajindoa mapema kama wapo.Msione mko kambini lakini taarifa za kila mmoa wenu zipo na zinafuatiliwa kwa muda wote, hivyo hakikisheni mnalinda heshima yenu na mnabaki kuwa wenye tabia njema,"amesema Muro.
Ametumia nafasi hiyo kueleza Arusha ni ndio kitovu cha utalii, hivyo anaamini kabisa mrembo atakaepatikana atautangaza mkoa huo pamoja na vivutio vya utalii vilivyopo.Kwa upande wake Meneja Itifaki wa mashindano hayo Basil Elias amesema kuwa mpaka sasa warembo wote wako kambini na wanaendelea na mazoezi.
Mrembo Anna Fanuel(23) akiwa anawapa elimu wanafunzi
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na warembo wanaowania Taji la Miss Arusha
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...