Kipa wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Mwadini Ally,
ameongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo.
Mwadini aliyeanza kuitumikia Azam FC tokea mwaka 2011 akitokea Mafunzo ya Zanzibar, amesaini mkataba huo rasmi leo mchana, akiwa mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat' na Mratibu wa timu, Phillip Alando.
Mchezaji huyo mwandamizi wa timu hiyo, anazidi kuongeza idadi ya wachezaji waliosaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Azam FC, wengine wakiwa ni mabeki David Mwantika, Bruce Kangwa, Abdallah Kheri na mshambuliaji Donald Ngoma.
Uongozi wa Azam FC chini ya Popat kwa kushirikiana na benchi la ufundi la timu hiyo, wanaendelea na zoezi la kuwabakisha wachezaji waliomaliza mkataba pamoja na usajili wa wachezaji wapya wa kuongeza nguvu kikosini kwa ajili ya msimu ujao.
Kikosi cha Azam FC kwa sasa kipo mapumzikoni na kinatarajia kurejea mazoezini Juni 20 mwaka huu, tayari kuanza maandalizi ya msimu mpya 2019/2020 ikianza na kibarua cha kutetea Kombe la Kagame (CECAFA Kagame Cup) kuanzia Julai 6 mwaka huu jijini Kigali, Rwanda.

Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Azam Fc Abdulkarim Popat akipeana mkono na kipa
Mwadini Ally baada ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea
kuitumia klabu hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...