Benki ya Exim Sasa Mdau Rasmi Uchangiaji Wa Damu Nchini
Kilimanjaro; Juni 3, 2019: Benki ya Exim Tanzania pamoja na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) wameingi kwenye makubaliano rasmi ya utekelezaji wa pamoja wa mpango wa uchangiaji wa damu utakaohusisha matawi yote ya benki hiyo hapa nchini. 

Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo ya uwajibikaji kwa jamii unaofahamika kama ‘Exim Cares’ 

Ushirikino huo umezinduliwa rasmi leo katika tukio la uchangiaji wa damu lililoandaliwa na benki hiyo kwenye tawi lake lililopo barabara ya Old Moshi katika Manispaa ya Moshi, mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni urasmishaji wa jitihada za benki hiyo kwa kipindi cha miaka minane mfululizo katika uchangiaji wa damu hapa nchini,. 

Akizungumzia mpango huo Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Staniley Kafu alisema unaenda sambamba na kauli mbiu ya benki hiyo inayosema “Exim kazini leo kwa ajili ya kesho” na kwamba unalenga kuchangisha damu na kutoa elimu ya umuhimu wa kuchangia damu katika mpango wa taifa.
“Kampeni hii ni sehemu ya uthibitisho kuwa benki ya Exim iko makini kutafuta njia za ubunifu za kuhudumia wateja wake na muhimu zaidi, inajitolea kuhakikisha inashiriki kuleta mabadiliko chanya katika jamii.’’ Alisema Kafu. 

Akizungumzia kuhusu makubaliano hayo na NBTS, Kafu alisema benki hiyo itawezesha mpango na utekelezaji wa uchangiaji damu kwenye kambi nane (8) za uchangiaji damu katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Tanga, Mtwara na Zanzibar huku ofisi ya Mpango wa Taifa Damu Salama wakisimamia masuala yote ya kitabibu katika mpango huo. 

“Zaidi benki ya Exim kwa kushirikiana wadau wote wa mpango huu wakiwemo Mpango wa Taifa Damu Salama , Wizara ya Afya na wadau wa habari tutahusika na kuratibu mikakati ya uelemishaji na uhamasishaji wa wananchi ili waweze kujitokeza kwa wingi katika suala hili muhimu kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya kuchangia damu Duniani.’’ Alisema Kafu 

Kwa upande wake Menaja wa NBTS Kanda ya Kaskazini Dk Edson Mollel alisema ofisi hiyo inahitaji kukusanya chupa (units) 526,000 za damu ili kukidhi mahitaji ya kila mwaka kwa nchi nzima ambapo kiasi kilichpatikana mwaka jana ilikuwa ni chupa 307,835 sawa na asilimia 58 ya mahitaji. 

“Mwaka huu lengo nikukusanya chupa 357,000 za damu na kupitia maadhimisho ya mwaka huu pekee tumejipanga kukusanya chupa 41,920 na ndio maana tunaridhishwa sana wanapojitokeza wadau kama benki ya Exim ili kutuunga mkono…uhitaji wa damu ni mkubwa.” 

“Hatua hii ni mfano wa kuigwa kwa kuwa benki ya Exim na wafanyakazi wake wanakuwa sehemu ya jamii wanayoihudumia kwa ukaribu zaidi na pia wanathibitisha rasmi mioyo yao ya kujitolea kwa hali na mali kwa jamii wanayoihudumia,’’ alisema 

Benki ya Exim imeendelea kuonyesha uwajibikaji wake katika kusaidia sekta ya afya kupitia mipango mbalimbali na miradi ya kijamii. Katika miaka minane iliyopita benki imechangia zaidi ya lita 100 za damu katika Benki ya damu taifa

Meneja wa Benki ya Exim Kanda ya Kaskazini Bw Amos Lyimo (Kushoto) pamoja na Meneja wa benki hiyo tawi la Moshi mkoani Kilimanjaro Bw Masood Abutwalib (Kulia) wakichangia damu ikiwa ni sehemu ya mpango wa benki hiyo wa uchangiaji damu kila mwaka kupitia matawi yake yote hapa nchini kwa ushirikiano na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS).Anaewahudumia ni mtaalamu wa afya kutoka NBTS Bi Marygoreth LaswaiTaarifa kwa vyombo vya habari

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim Tawi la Moshi pamoja na wateja wa benki hiyo wakiendelea taratibu za uchangiaji wa damu uliofanyika kwenye kwenye viunga vya tawi la benki hiyo Manispaa ya Moshi leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...