Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa
Zanzibar Zahran Ali Hamad akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa
Tathmin ya Dawa huko Bohari Kuu ya Dawa Maruhubi nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar (Kulia) Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Halima Salum na
Mratibu wa Huduma za Ushaurinasaha na Uchunguzi wa Virusi vya Ukumwi
Tatu Bilali

Afisa kutoka Ofisi ya Mfamasia
Mkuu wa Serikali Said Mohamed akieleza mpango mkakati wa dawa katika
mkutano wa tathmini uliyofanyika Bohari Kuu ya Dawa Maruhubi nje kidogo
ya Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa
Zanzibar Zahran Ali Hamad akiwatembeza washiriki wa mkutano wa tathmini
ya dawa baada ya kumaliza mkutano wao wa siku moja maelezo. (Kushoto) ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Halima Salum.

Meneja Bohari Kuu ya Dawa
Zanzibar Lydia Zungufya akiongoza washiriki wa mkutano wa tathmini ya
kuangalia uhifadhi wa dawa kabla ya kupelekwa hospitali na vituo vya
afya.
*****************
Na Ramadhani Ali – Maelezo 27.6.2019
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Halima Maulid Salum ameshauri kuongeza ushirikiano baina ya watendaji wa
Taasisi zilizomo ndani ya Wizara hiyo na Halmashauri za Wilaya katika
kufanikisha usambazaji wa dawa kwenye vituo vya afya baada ya Serikali
kufanya ugatuzi katika huduma za afya ya msingi.
Amesema suala la ugatuzi ni kitu
kipya kwa Zanzibar, na watendaji wengi bado hawajauelewa vizuri, hivyo
suala la ushirikiano na ufuatiliaji wa mara kwa mara ni jambo la msingi
katika kufikia malengo ya kuanzishwa kwake.
Naibu Katibu Mkuu alitoa ushauri
huo Bohari Kuu ya Dawa Maruhubi katika mkutano wa kutathmini utaratibu
mzima wa uagiziaji, uhifadhi na usambazaji wa dawa katika hospitali na
vituo afya.
Alisema kumejitokeza malalamiko
kwa baadhi ya Halmashauri za Wilaya, hawatoi ushirikiano mzuri kwa
Wafamasia wa Wilaya zao na hatimae baadhi ya vituo hukosa dawa na
vyengine kuwa na mrundikano mkubwa wa dawa bila kuwa na matumizi na
hatimae kumaliza muda wa matumizi.
Alisema upatikanaji wa dawa
Zanzibar hivi sasa upo vizuri kufuatia Wizara ya Afya kuongezewa bajeti
ya kununulia dawa na jambo la msingi ni kuhakikisha zinatunzwa vizuri
zinapofika kwenye vituo vya afya.
Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa
Zanzibar Zahran Ali Hamad amewahakikishia wadau wa Dawa walioshiriki
mkutano huo kwamba wataendelea kutoa huduma bora kwa wakati kwenye
hospitali na vituo vyote vya afya Unguja na Pemba.
Hata hivyo aliwataka wananchi
wanapopata tatizo la afya kufika hospitali na vituo vya afya na
kuhakikisha dawa wanazopewa wanazitumia kwa usahihi.Alisema baadhi ya wananchi
huchukuwa dawa na kuzitumia kwa muda mfupi na baada ya kupata nafuu
huzitupa bila ya kujua kwamba Serikali imetumia fedha nyingi kuziagiza.
Aidha aliwataka wafanyakazi wa
Bohari Kuu kuendelea kutimiza wajibu wao wa kuhudumia jamii ya Zanzibar
kwa uadilifu na mapenzi makubwa.
Mkutano huo wa siku moja wa wadau
wa dawa uliangalia mafanikio yaliyofikiwa katika mfumo mzima wa dawa,
changamoto na njia za kupunguza changamoto zilizojitokeza na njia za
kuzitafutia ufumbuzi changamto hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...