Mkuu wa wilaya Tandahimba Mhe Sebastian Waryuba Leo Jumanne Juni 25, 2019 ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Zahanati mpya ya Mitondi iliyopo Kijiji cha Mitondi B kata ya Kitama na kuzungumza na Wanakijiji ambapo amehaidi kutoa mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya kusaidia mradi huo wa ujenzi.
DC Waryuba ametoa ahadi hiyo kupitia mkutano na Wananchi uliofanyika kwenye Zahanati hiyo jambo ambalo liliibua shangwe kwa Wakazi hao.
"Natoa mifuko 30 ya saruji. Mkiwa tayari mje kuichukua wakati wowote ule." Alisema DC Waryuba huku akishangiliwa na Wananchi.
Pia Ndugu Khasim S. Lihumbo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba alisema Zahanati hiyo imetengewa Tsh. Milioni 37 kwa kila Mwaka wa fedha kuanzia 2018/19 na 2019/2020 kwa ajili ya kuikamilisha na ianze kazi mara moja.
Katika ziara hiyo DC Waryuba aliambatana na Katibu Tawala wilaya Tandahimba Ndugu Benaya Kapinga, Mwakilishi Mkurugenzi Ndugu Khasim Lihumbo, Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu na kupokelewa na wenyeji wao Halmashauri ya Serikali ya Kijiji cha Mitondi B.
Mkuu wa wilaya Tandahimba Mhe Sebastian Waryuba akizungumza na wanamchi alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Zahanati mpya ya Mitondi iliyopo Kijiji cha Mitondi B kata ya Kitama
Mkuu wa wilaya Tandahimba Mhe Sebastian Waryuba akikagua mradi wa ujenzi wa Zahanati mpya ya Mitondi iliyopo Kijiji cha Mitondi B kata ya Kitama
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...