Na Verediana Mgoma 

KIKUNDI cha MKULIMA JEMBE kilichopo Kijiji cha Kastam, Kata ya Bukima kilianzishwa Mwaka 2014 kikijishughulisha na uoteshaji wa miche badaae walifanikiwa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji wakilimo cha mbogamboga, matunda pamoja na mazao ya chakula ikiwemo viazi vitamu, maharage na mahindi.

Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Ndugu Festo Obed ameeleza kuwa kupitia kilimo cha umwagiliaji wamefanikiwa kununua Mashine/Pampu ya Umwagiliaji ya SOLAR, kusomesha Watoto wao na kujikimu kwenye matumizi mengine ya kifamilia. Fedha zao zinatunzwa Benki. 

Aidha, Obed ameeleza kikundi cha MKULIMA JEMBE kimefanikia kuanzisha Kikundi kingine kiitwacho "TUMETAMBUA" ambacho kinajishughulisha na Kilimo cha Umwagiliaji na kina Mradi wa kuweka na kukopeshana.

Afisa Kilimo wa Kata ya Bukima, Ndugu Mushangi Salige ameeleza kuwa Kata hiyo ina fursa kubwa ya kupanua KILIMO cha UMWAGILIAJI kwa sababu Wakazi wengi wapo kando kando mwa Ziwa Viktoria. 

Afisa Kilimo huyo amemshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kwa kuwezesha Kikundi cha mkulima jembe kupata Vifaa vya Umwagiliaji (pampu na mipira) kutoka mfuko wa jimbo Kikundi hicho na vingine Jimboni viligawiwa bure mbegu za Mbogamboga na Matunda.

Vilevile Wanavijiji wa Kata hiyo ya Bukima wanamshukuru sana Mbunge wao Prof Muhongo kwa kuwagawia Mbegu za alizeti,mtama na mihogo amesema Afisa Kilimo huyo.
Wanachama wa Kikundi cha mkulima jembe wakiwa kwenye Shamba lao la matikiti katika Kijijini Kastam, Kata ya Bukima musoma vijijini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...