Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
SERIKALI mkoani Pwani, amewaagiza wakuu wa wilaya mkoani humo, kuhakikisha wanaanza utekelezaji wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ulioboreshwa (CHF)kuanzia sasa na ifikapo Julai 31 mwaka huu apewe taarifa juu ya utekelezaji huo kwa halmashauri zote.
Aidha amewahamasisha wananchi, kujiunga na CHF iliyoboreshwa kwa sh.30,000 kwa familia ya watu sita, badala ya 10,000 ya awali ili kupata matibabu kirahisi kwa kipindi cha mwaka mzima.
Akizindua utekelezaji wa mfuko huo kwa mkoa wa Pwani, Miono Bagamoyo, mkuu wa mkoa huo,mhandisi Evarist Ndikilo alieleza hataki kusikia visingizio hivyo ifikapo Julai 31 utekelezaji uanze kwa kila wilaya.
"Ila isiwe tena hamasa hii ikaachiwa kwa wakuu wa wilaya pekee kisa nimewaagiza hapana, hamasa hii ikafanyike kwa madiwani,maofisa tarafa,wenyeviti wa vijiji,kata,mitaa,watendaji na wadau waelimishe wananchi katika vijiji ,kata,tarafa na mitaa yao"alifafanua Ndikilo.
Mkuu huyo wa mkoa alisema, mikoa ya Shinyanga,Dodoma na Morogoro
imeshafanikiwa sana hivyo na mkoa wa Pwani ni zamu ya kuhamasisha ili
watu wajiunge kwa wingi .
"Kiwango hicho cha 30,000 ambacho ni kama 5,000 kwa kila mmoja kwa
wanafamilia sita kitasaidia kutibiwa mwaka mmoja kuanzia ngazi ya
zahanati,hospitali ya wilaya na hospitali ya mkoa badala ya zamani
ambapo 10,000 ilikuwa ukitibiwa katika kituo na kijiji ulipo pekee"
"Magonjwa hayapigi hodi tusiweke rehani maisha yetu kwa kuona 30,000
ni kubwa ,tulinde afya zetu ,alisema Ndikilo.
Ndikilo aliongeza, katika kukabiliana na changamoto zilizokuwepo
kipindi cha nyuma na kuzingatia utekelezaji wa ilani ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) 2015-2020 na mipango mkakati wa sekta ya afya
2015-2020
serikali imeweka mkakati ikiwemo kuongeza bajeti katika sekta ya afya
hususan kwenye vifaa tiba na dawa.
"Kwa hili, sisi mkoa wa Pwani, bajeti yetu ni zaidi ya bilioni mbili
tumepokea 2018-2019 kwajili ya dawa na vifaa tiba ili kuboresha sekta
hiyo'"aliweka bayana.
Pia ameelekeza, serikali ya kijiji cha Miono kata ya Miono
Bagamoyo,kumthibitishia majina ya wajane na wagane wote waliopo katika
kijiji hicho ili awalipie kujiunga na mfumo huo .
Awali meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) Mkoani
Pwani,Ellentoruda Mbogoro
aliwatoa shaka wananchi na kuwaomba wasikate tamaa kwani kwa sasa
vifaa tiba na dawa zitakuwepo za kutosha katika vituo vya afya na
hospital.
Mkazi wa kijiji cha Miono ,Fatma Mrisho alisema mpango huu ni mkombozi
hasa kwa kaya zilizo na maisha duni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...