Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akirusha mpira wakati lipoanzisha mechi ya mpira wa kikapu ya Bonanza na Benki ya NMB na Wabunge kati ya timu ya Bunge na NMB kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Bunge wakiwa wamejipanga kabla ya mechi kati yao na timu ya Benki ya NMB kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua timu ya Mpira wa kikapu ya Benki ya NMB ambayo ilipambana na timu ya Bunge katika mechi la Bonanza la Benki ya NMB na Bunge kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 



WATUMISHI NI MUHIMU KUSHIRIKI MICHEZO-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ni muhimu kwa watumishi kushiriki katika michezo mbalimbali kwa kuwa inaimarisha afya pamoja na kudumisha mshikamano.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Juni 22, 2019) wakati wa bonanza kati ya Wabunge na watumishi wa benki ya NMB lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema mbali na kuimarisha afya kwa watumishi na wabunge, pia michezo inasaidia katika kuimarisha mshikamano baina ya benki hiyo pamoja na wateja.Akizungumzia kuhusu utendaji wa benki ya NMB, amesema imekuwa ikishirikiana na Serikali kuwaelimisha wakulima umuhimu wa kufungua akaunti na kujiwekea akiba.

“Benki ya NMB ni benki pekee iliyomudu kufungua matawi hadi maeneo ya vijijini, hivyo kurahisha upatikanaji wa huduma kwa watumishi na wananchi waishio maeneo hayo.”Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni mpira wa miguu ambapo timu ya Bunge ilishinda baada ya kuifunga timu ya benki ya NMB magoli matano kwa matatu. 

Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete timu ya Bunge iliibuka na ushindi baada ya kuifunga timu ya NMB magoli 25 kwa 18, huku katika mchezo wa mpira wa kikapu timu ya NMB ilishinda baada ya kuifunga Bunge vikapu 52 kwa 51.

Katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya Wabunge Wanawake na Wanaume waliibuka na ushindi baada ya kuzishinda timu za NMB.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...