Tanzania Disc Music association (TDMA) Inapenda kuchukua fursa hii adhimu kuwafahamisheni kuwa imeandaa mashindano ya Taifa ya kucheza muziki Taifa ngazi ya mkoa wa Dar es salaam ( Boogie Dance 2019) yanayotarajiwa kuzinduliwa mapema siku ya jumapili ya tarehe 16/6/2019 kwenye ukumbi wa wa kisasa wa kimataifa wa burudani wa Life club uliopo Mwenge jijini Dar es salaam.
Mashindano hayo ambayo yameandaliwa yenye lengo la kuibua na kukuza vipaji vya madansa ( Dancers) ambavyo vimefichika majumbani na mitaani ili kuweza kuwapatia fursa ya kuonyesha vipaji vyao ambavyo vitakuwa ni mtaji wa kuwaingiza kwenye soko la ajira kupitia vipaji vyao, pia kuwaongezea uelewa ili wajitambue kuwa wao ni sehemu kundi maalimu la kitanzania na vipaji vya fani yao ni sehemu ya ajira ya kujipatia kipato cha halali vitakavyowawezesha kukidhi adhima ya taifa ya kujitegemea na kuhamasisha wakazi wa mkoa wa Dar es salaam kujiunga na Bima ya afya
Mashindano hayo yatawashirikisha washiriki toka katika wilaya za Temeke, Kinondoni, Ubungo, Ilala na Kigamboni, Pia kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam washiriki hao wataelimishwa kufuata kanuni za uchezaji wa muziki ambazo ni nidhamu, unadhifu, uchangamfu, kulitawala jukwaa, kufuatisha mapigo ya muziki na kuvaa mavazi yanayoendana na maadili ya Taifa
Ambapo mpaka hivyi sasa ni benki ya Taifa ya Biashara NBC pekee ndio wameonyesha nia ya kudhamini.
Ambapo zawadi zinazotalajiwa kutolewa na Benki hiyo Ya NBC ni
Mshindi wa Kwanza sh 1,000,000/= taslimu na kombe
Mshindi wa pili sh 500,000/= taslimu
Mshindi wa Tatu sh 300,000= taslimu
Mshindi wa nne sh 150,000/= taslimu na
Mshindi wa tano sh 100,000/= taslimu
Sanjali na hilo pia siku hiyo itajumuishwa na kusherehekea siku ya madj Dunia ambapo madj mbalimbali toka katika club mbalimbali kwenye road show, kwenye bar kwenye vikundi mbalimbali kama vile Simba Scratch dj academy, Peramiho dj na madjs toka katika vituo mbalimbali vya Radio na luninga wataonyesha umahiri wao wa kuchezesha muziki pia mpaka hivyi sasa washiriki zaidi ya 100 tayari wameshajitokeza kujiandikisha kushiriki mashindano hayo pia TDMA Inaishurukuru NBC kujitokeza kuinua vipaji na kupata ajira mashindano Mayo yatakuwa na shoo za utangulizi toka kwa wasanii wa Hip hop Bongofleva, wasanii wa Nyimbo za asili pamoja na wasanii watakao igiza wasanii nyota duniani akiwemo Michael Jackson wa Tanzania pia na washindi mbalimbali waliowahi kushiriki na kushinda mashindano ya Taifa na ya Afrika mashariki wakiongozwa na madj mahiri hapa nchini watasindikiza mashindano hayo yatakaozindiliwa siku hiyo
ratiba ya mashindano itakuwa_
_tarehe16/6/2019 Uzinduzi_
tarehe 23/6/2019 raundi ya kwanza
tarehe 30/6/2019 raund ya Pili
tarehe 7/7/2019 raundi ya Tatu
tareje 14/7/2019 robot fainali
tarehe 28/7/2019 fainali
Ahsanteni
Asanterabbi Mtaki
Katibu Mkuu
TDMA Taifa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...