MEYA mstaafu wa Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Yusuph Mwenda ameahidi kugharamia mafunzo kwa ajili ya walimu wa madrassa zilizopo katika wilayani humo ikiwa ni maalumu wa kuwaongezea ujuzi ili kuongeza tija katika kueneza dini hiyo.

Meya Mwenda ametoa ahadi hiyo wakati wa futari aliyoiandaa maalumu kwa ajili ya walimu hao, wakiwemo maustadhi na Masheikh wa Misikiti iliyopo katika wilayani Kinondoni , akiitikia ombi la Sheikh wa Wilaya ya Kinondoni Mohammed Mhenga aliyemuomba kufadhili mafunzo hayo.

Katika futari hiyo aliyokuwa ameiandaa katika makazi yake Mikocheni Dar es Salaam, Mwenda amesema mafunzo kwa walimu hao ni jambo asiloweza kulipa ugumu kwa kuwa anatambua thamani yao na hasa katika uenezaji na uendelezaji wa dini hiyo.

“ Natambua kazi nzuri mnayoifanya katika kufundisha dini ya Uislam hasa kwa watoto wetu na jamii ya watu wengine, nimelipokea suala hili na nipo tayari kushirikiana nanyi wakati wowote mtakaponiambia kuwa mpo tayari” amesema Mwenda.

Aidha ameongeza kitendo chake na kuwaalika walimu hao na kufuturu nao pamoja, kimelenga kuwatambua na kuthamini mchango wao mkubwa wanaoutoa kuiendeleza Quran ambayo ilishushwa ndani ya mwezi wa Ramadhan maalumu kwa ajili ya waumini wa dini ya kiislam pamoja na waamini wengine.

“Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayoifanya kuindeleza dini hii, kwa hakika mnabeba thawabu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, naamini siku moja atawalipa kama siyo hapa duniani basi akhera” ameeleza Meya huyo Mstaafu.

Awali Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mohammed Mhenga mbali na kumpongeza Mwenda kwa hatua yake ya kufuturu na walimu hao, amewataka walimu hao kuzidisha elimu wanayoitoa kwa vijana kwa lengo la kuzidi kuieneza dini hiyo.

Pia amesema kumalizika kwa mwezi mtukufu kusiwafanya waislam kubadirika na kugeuka kutenda matendo yenye kumchukiza Mungu na badala yake waendelee kusimama kikamilifu na kumuabudu mwakati wote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...