Na: Moshy Kiyungi,Dar es Salaam
Wapenzi wa muziki wa kizazi kipya duniani hususan Afrika, kundi la P-Square limeshika nafasi ya simulizi kufuatia kazi zao kukubalika.
Vijana hao wawili wa toka nchini Nigeria, Peter Okoye na Paul Okoye wanaounda kundi maarufu linalojulikana kama P-Square.
Vijana hao wanaelezwa kuwa licha ya kufanya muziki, ni wafanyabiashara wakubwa wa mafuta.Historia ya mapacha Peter na Paul inaeleza kuwa walizaliwa Novemba 18, 1981 jijini Lagos, Nigeria.
Walianza masomo katika shule ya sekondari ya Mtakatifu Murumba ambayo ilikuwa ni shule ndogo ya Kikatolic huko Jas, nchini Nigeria.Mapacha hao walijiunga na shule ya muziki pamoja na maigizo ambapo walikuwa wakiimba na kucheza kwa kuwaiga akina Machael Jackson, MC Hammer na Bobby Brown.
Mwaka 1997 walianzisha kundi lililojulikana kwa jina la Smooth Criminal ambapo walikuwa wanacheza ‘Break dansi’.Kundi hilo lilianza kama kigenge cha mtaani kilichojulikana kwa majina ya MMMPP (M Clef a.k.a. Itemoh, Michael, Melvin, Peter and Paul).
Mnamo mwaka 1999 vijana hao Peter na Paul, wakaingia rasmi katika masomo ya muziki kuongeza ujuzi wao na kujifunza kupiga Gitaa pamoja na ngoma.Kazi zao za muziki zilianza kuingizwa katika filamu kama Tobi, Mama Sunday, Moment of Bitterness pamoja na Evas River.
Mwaka huo huo wakajiunga na Chuo Kikuu cha Abuja kusomea masuala ya Business Administration.Kwa bahati mbaya kujiunga na chuo hicho kulipelekea kundi lao la Smooth Criminal, kusambalatika kwa sababu M Clef, Michael na Melvin walisoma vyuo tofauti na wao.
Lakini vijana hao Peter na Paul hawakukata tamaa, wakaamua kuunda kundi lao jingine la watu wawili lililojulikana kama "Double P" ambalo nalo baadae jina la kundi hilo lilibadilika mara mbili ambapo liliitwa "P&P" na "Da Pees" na kundi ilo lilipotulia zaidi ndipo likajiita P-Square ambalo liliongozwa na Promota Bayo Odusami aka Howie T.
Mwaka 2001 P-SQUARE walijishindia katika mashindano yaliyojulikana kama "Grab Da Mic" kitendo ambacho kiliwavutia watu wengi mpaka Benson & Hedgesiliyoamua kuwadhamini katika album yao ya Last Nite ambayo iliachiwa na lebo ya Timbuk2 music.
Pia mwaka 2003 walishinda tena katika mashindano ya Amen, kama kundi bora la muziki wa R&B. Mwaka 2005 wakaachia album yao ya pili ya Get Squared chini ya lebo yao Square Records.
Album hiyo ilisambazwa kimataifa na TJoe Enterprises, ingawa walikuwa bado wanaongozwa na Howie T na video ya album yao ya pili ikachukua nafasi ya kwanza katika MTV Base kwa wiki kadhaa. Kundi lao likaweza kuwashirikisha wasanii wengine wa kimataifa kama Ginuwine, Sean Paul, Akon and Busola Keshiro.
Mwaka 2007 wakaachia album yao Game Over ambayo iliwaingizia pesa nyingi baada ya kuuza nakala milioni 8 Kimataifa. Mwaka 2009 wakaachia album yao ya nne Danger ambapo katika album hiyo waliweza kuwashirikisha akina 2Face Idibia, J Martins pamoja na Frenzy.
Mwezi April 04, 2010 wakaitwa wasanii wa mwaka katika KORA All Africa Music Shughuli za utoaji tuzo hizo zilifanyika katika mji wa Ouagadougou, nchiniBurkina-Faso. Ambako walijishindia Dollars milioni 1.
P-Square waliweza kurekodi video pamoja na mwanamuziki machachari toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Awillo Longomba.
Mapacha hao wa kufanana, Peter na Paul Okoye, wametangazwa kushika nafasi ya Pili kwa utajiri nchini mwao.
P-Square walifanikiwa kuuza kila album waliyotoa kwa mauzo ya juu yakichagizwa na maonesho mbalimbali wanayofanya na kupelekea wakajitangaza zaidi Duniani.Aidha waliwashirikiana Wasanii wakubwa kama vile Akon, ikapelekea wasanii hao kutangazwa Wasanii bora wa mwaka 2010 kupitia Tuzo za Kora.
Vijana hao wanautajiri unaosemekana ni zaidi ya $3 million huku wakimiliki eneo lenye thamani kubwa nchini Nigeria la Square ville.Wanamiliki mali zenye thamani kubwa yakiwemo magari, ndege aina ya Airbus, waliyoinunua kwa ajili ya kusafiria kutoka katika moja ya Kampuni za Arabuni.
Peter na Paul Okoye, wanamiliki mali mbalimbali katika miji ya Jos na Port Harcout, likiwemo jumba la kifahari lenye thamani ya Naira milioni 400 lililopo katika mji wa Lagos.
Peter na Paul wametajwa kuwa ndio wanamuziki tajiri kuliko wote nchini Nigeria kwa sasa, wakiwa wamerekodi na kuuza albamu kadhaa sehemu mbalimbali duniani.
Wameingizwa kwenye klabu ya Mabilionea wa Nigeria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...