Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amewakabidhi wachezaji wa Simba kitita cha shilingi milioni 24 kama sehemu ya zawadi na hamasa kufuatia Timu hiyo kuchukuwa ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara na kuingia katika robo fainali ya Klabu bingwa Afrika.

RC Makonda amewataka wachezaji hao kutumia fedha hizo kuanzisha miradi ya maendeleo itakayowasaidia kujipatia  kipato pindi watakapostaafu mpira huku akiwataka kutumia umaarufu na Brand zao kujiingizia kutengeneza kipato.

Aidha RC Makonda amesema katika mgawanyo wa fedha hizo Golikipa wa Simba Aish Manula amepokea kiasi cha Shilingi Milioni10, Wachezaji tisa Milioni 1 kila mmoja, Mchezaji bora wa kike wa Simba Queen Milioni 2 na Msemaji wa Simba Haji Manara ambae amepatiwa Milioni 3 kama sehemu ya kutambua mchango wake kwenye uhamasishaji wa mashabiki kujaa uwanjani.

Pamoja na hayo RC Makonda amewaasa wachezaji kuongeza morali ya uchezaji ili waendelee kunyakua ubingwa na kushika nafasi za juu katika ligi za kimataifa.

Hata hivyo RC Makonda amewataka wachezaji kuchukulia michezo kama pesa,uchumi, Amani na biashara inayoweza kuwafanya hao binafsi wanufaike kiuchumi na kulipatia taifa mapato ya kutosha kupitia mapato yanayoenda kwenye manispaa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...