Na Emmanuel Madafa, MBEYA

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amebatilisha uhamisho wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Dk. Mariam Ngwere uliofanywa na Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwenda katika Halmashauri ya Wanging'ombe mkoani Njombe kwa madai  kuwa uhamisho huo umeibua sintofahamu ikiwa pamoja na malalamiko  toka Kwa wananchi wakiwemo Madiwani wa Halmashauri hiyo.

Alitangaza uamuzi huo leo  Juni 27 kwenye Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Kyela kilichoitishwa kwa ajili ya Kupitia na kujadili hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Chalamila alisema atawasiliana na Katibu Mkuu wa Tamisemi ili amshauri asitishe uhamisho huo na kwamba kama kuna ulazima wa mtumishi huyo kuhamishwa basi ni bora apandishwe cheo.

"Hatukatai watumishi wa umma kuhamishwa maana ni haki ya mtumishi yeyote kufanya kazi popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunachopinga ni uhamisho wenye mashaka, hivyo mimi kama Mkuu wa Mkoa siwezi kuwa laini kama mlenda natangaza kuanzia muda huu uhamisho huo ni batili," alisema Chalamila.

Aliwataka watumishi wa Halmashauri hiyo pamoja na madiwani kuungana na kuacha kuendekeza migogoro isiyokuwa ya lazima kwa maelezo kuwa migogoro hiyo inakwamisha shughuli za maendeleo.

Wakati huo huo Chalamila ameitaka halmashauri hiyo kuongeza jitihada zaidi katika kuongeza uwezo wa kujitegemea badala ya kuitegemea serikali kuu kama ambavyo ilivyo sasa ambapo inategemea kwa asilimia 90.4 katika kutekeleza shughuli za maendeleo kwa mujibu wa takwimu  2017-18.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...