Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martini Shigella amesema umefika wakati kwa jamii kushiriki kikamilifu kukomesha biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Akizungumza leo Juni 25,2019 wakati anafungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Tanga, Shigella amesema athari za dawa za kulevya ni tatizo la jamii nzima, hivyo kuna kila sababu ya kuhakikisha sote wote tunashiriki kukomesha matumizi ya dawa za kulevya.

"Maelezo ya awali ambayo yametolewa na Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibi na Kupambana na Dawa za Kulevya Valite Mwashusa yameonesha ukubwa wa tatizo la dawa za kulevya , na kwamba dawa za kulevya limeendelea kuwa tatizo kubwa na limeathiri jamii,"amesema Shigella.

Amefafanua kwa Mkoa wa Tanga kuna dawa za aina ya bangi, Heroine na Cocain na kwamba ukiangalia takwimu utabaini bado matumizi ya dawa za kulevya ni makubwa.

Ameeleza takwimu zinaonesha mwaka 2016 kulikuwa na kesi 331 na kati hizo kesi zaidi ya 381zimetolewa hukumu na waliohusika kuhumiwa kufungwa jela au kunyongwa.

Wakati kwa mwaka 2017 Shigella kulikuwa na kesi 221 ambazo zilihusisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilogramu 1,584 na watu zaidi ya 2945 walihusishwa na kwamba ukifuatilia mtiririko wa takwimu kesi za dawa za kulevya zimepungua sana.

"Kwa Mkoa wa Tanga moja ya changamoto ni uwepo wa dawa za kulevya kwenye mitaa mbalimbali na jamii inawajua wanaohusika na wanaojihusisha na dawa hizo.Hata hivyo jamii bado jamii bado haijaona umuhimu wa kushirikiana na vyombo vya ulinzi kwa kutoa taarifa.

"Umefika wakati kwa jamii kutoa ushirikiano kwa kuhakikisha wanaojihusisha na dawa za kulevya wanabainishwa na kuchukuliwa hatua. 
"Kwa kufanya hivyo tutaokoa jamii ya Watanzania kwani matumizi ya dawa za kulevya yamekuwa yakisababisha madhara mengi yakiwemo ya jamii kupotea kwa nguvu kazi ya Taifa,"amesema.

Amesisitiza kuwa ni wakati muafaka sasa kwa wananchi wote kujipanga vizuri kukomesha dawa za kulevya.Amezungumzia zaidi kuhusu dawa za kulevya amesema ni tatizo kubwa na kutoa mfano kuwa katika nchi jirani ya Kenya Mirungi imeruhusiwa na inauzwa sokoni lakini kwa Tanzania ni marufuku, hivyo ametoa rai kwa jamii kuhakikisha dawa za kulevya haziingii.

Pia amesema Serikali ya Awamu ya Tano imejidhatiti kuhakikisha nchi ya Tanzania inakuwa salama na kukomesha biashara ya dawa za kulevya na ndio maana Rais Dk.John Magufuli aliamua kuanzisha Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.

"Sote ni mashahidi hivi sasa hata wale waliokuwa mapapa wa biashara za dawa za kulevya leo hawasikiki na hawaonekani kabisa maana wamedhibitiwa.Kwa Mkoa wa Tanga tumejipanga vema kuhakikisha tunaendelea kudhibiti dawa za kulevya,"amesema.

Kuhusu maadhimisho hayo, Shigela amewataka wananchi wa Jiji la Tanga kuhakikisha wanafika kwenye maonesho hayo ambayo yanafanyika Viwanja vya Tangamano kwa lengo la kujifunza kwani kuna mabanda ambayo yanatoa elimu mbalimbali kuhusu dawa za kulevya nchini na madhara yake.

Pia ameseme kuna kila sababu za nyumba za kutibu walioathirika na dawa za kulevya wanashirikiana na taasisi nyingine ikiwemo taasisi ya fedha kuhakikisha waliokuwa wanatumia dawa za kulevya na kupata nafuu wanashirikishwa kikamilifu kwenye shughuli za ujenzi wa nchi yetu.

 Mkuu wa Tanga Martin Shigella (aliyeva suti) akikapata maelezo  kwenye moja banda lililopo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika Jiji la Tanga.Kushoto  ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya   Valite Mwashusa
Kaimu Kamishna Jeneral wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Valite Mwachusa (kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga wakati anatembelea maganda yaliyopo katika maadhimisho ya siku ya dawa za kulevya Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika Jiji la Tanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...