Hussein Stambuli, Morogoro
SERIKALI inampango wa kuboresha sera ya mbegu ili kuimarisha suala la upatikanaji wa mbegu zitakazowasadia wakulima na kuleta tija katika kilimo nchini.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Profesa Raphael Chibunda kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mathew Mtigumwe wakati akifunga mdahalo wa mbegu wa siku mbili uliohusisha wataalamu wa mbegu, wazalishaji, wasimamizi, wauzaji na wakulima ulioandaliwa na Wizara ya Fedha Tanzania kupitia mradi wa mabadiliko ya tabia nchi uliofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya.
“kwa sasa Serikali inafanya mapitio ya sera za kilimo ambapo tumeibua mjadala wa masuala ya kuboresha sera ya mbegu na Wizara itayachukua na kuboresha sera ambazo zitatekelezwa ili kuimarisa upatikanaji wa mbegu bora ambazo wakulima watakuwa na uwezo wa kuzinunua ili kuboresha kilimo nchini” alisema Prof. Chibunda
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Udhibiti wa ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) Patrick Ngwediagi kwa niaba ya wataalamu wa mbegu walioshiriki mdahalo huo na kutoa mapendekezo yao, aliiomba Serikali na wadau wa mbalimbali kuchukua hatua stahiki zitakazowezesha kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi hasa kwenye upatikanaji wa mbegu zinazokabiliana na hali hiyo.
Pia alisema, wameazimia kuwe na juhudi kubwa za kuboresha upatikanaji wa mbegu ikiwa bora kwa kupitia sheria zilizopo ambapo inapaswa udhibiti wa ubora wa mbegu uimarishwe ili wakulima wanufaike na wanachokipanda.
wataalamu wa mbegu walioshiriki mdahalo wakifuatilia kinachoendelea katika mkutano huo mkoani morogoro
wataalamu wa mbegu walioshiriki mdahalo wakifuatilia kinachoendelea katika mkutano huo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...