Na Khadija Seif, Michuzi TV
MSANII wa muziki wa Kizazi Kipya anayetengeneza kundi la Wasafi Classic (WCB) Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz amesema hakutegemea mapokezi ya kanyaga. Daimond Platinum amesema mwaka huu umekua ni wa mafanikio makubwa kwake kutokana na nyimbo zake alizoziachia kupokelewa vizuri na mashabiki zake wa ndani na nje ya nchi. 
"Mwanzoni mwa mwezi Mei niliachia "The one" na badaae nikaamua nihamie kwenye midundo ya bolingo ambapo niliachia ngoma ya "INAMA" niliyomshirikisha Fally Ipupa kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na ilipokelewa vizuri sana na mwezi huu nimeachia "KANYAGA" ambayo pia imepokelewa vizuri sana na mashabiki," 
Aidha amesema ni baraka kupata Rais Dkt. John Pombe Magufuli anayejali, anaependa sanaa na hata hivyo ameendelea kuboresha kila sekta hasa kwenye upande wa usafirishaji ameleta ndege na amehakikisha kila mkoa kuna kuwa na viwanja vya ndege ili wasanii waweze kuwafikia mashabiki zao kwa wakati muafaka. 
"Kuna vitu vingine Serikali ikivifanya watu wanavitafsiri vibaya na kuona kwa jicho la tofauti na ndiyo maana ndege zilivoletwa ilionekana Kama Serikali ya awamu ya tano inamaliza pesa kwenye kununua ndege lakini umuhimu wake unaonekana kwa sasa kutokana na usafiri unakua sio wa tabu tena,". 
Diamond Platnumz ametangaza rasmi kuwa Tamasha la Wasafi limezinduliwa rasmi na kwa mwaka huu litaanza kufanyika Julai 12 Muleba mkoa wa Kagera, Julai 14 mkoa wa Tabora huku ikifuatiwa na mkoa wa Iringa Julai 20 mwaka huu . 
"Nina hamu sana na kufanya show Muleba kwani sijawahi kukutana na mashabiki zangu, hata hivyo sababu ya kuchagua mkoa wa Iringa ni kutokana na mapokezi yao mazuri kwa misimu iliyopita," amesema. 
Pia amewataka mashabiki wategemee vitu vingi vizuri na vya tofauti kwa msimu huu wa nne wa tamasha la wasafi kuanzia jukwaa, mavazi, muziki na wasanii watakaotumbuiza.
MKurugenzi na Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya anayetengeneza kundi la Wasafi Classic (WCB) Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kuanza kwa Tamasha la Wasafi linalotarajia kufanyika hivi karibu katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania.
Meneja wa Msanii Diamond Platnum Hamis Tale a.k.a Babu Tale akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Wasafi linalotarajia kufanyika hivi karibuni.
Mmoja wa wakilishi wa WCB,Meneja Said Fella akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Wasafi linalotarajia kufanyika hivi karibuni.
Mwakilishi wa BASATA, Prona Masenge akizungumza machache.
Mratibu wa Masuala ya vijana TACAIDS, Grace Kessy akifafanua jambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...