Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha.

 Baadhi ya watu jijini Arusha wamebainika kuharibu miundombinu ya Tanesco kwa waliochakachua mita za umeme lengo  ikiwa ni kukwepa kulipa malipo stahiki ya huduma za umeme hivyo kulisababishia hasara shirika hilo.

Hayo yamebainika Katika Operesheni maalumu iliyofanywa na Tanesco ambapo wamekagua zaidi ya mita 1000 na kubaini Kasoro anazozifafanua Afisa Ukaguzi wa Mita  Zuberi Hassan amesema kuwa baada ya kufanya ukaguzi huo wamebaini mita kadhaa ambazo zimechezewa ili zisiweze kusoma vizuri matumizi ya umeme jambo ambalo ni hujuma kwa shirika hilo.

Mmiliki wa eneo ambalo lilikaguliwa na kukutwa na tatizo la mita kuchakachuliwa ,Joseph Shirima   amesema kuwa tatizo hilo lilisababishwa na baadhi ya wapangaji wasio waaminifu kufunga mita zao hivyo atashirikiana na shirika hilo ili kuhakikisha mita zinazowekwa zina kuwa na usahihi.

Meneja wa wateja wakubwa Tanesco  Mhandisi Frederick Njavike  amesema kuwa shirika hilo limefanya ukaguzi wa mita zaidi ya 1000/ katika maeneo mengi jijini Arusha ili kujiridhisha na mita zilizopo pamoja na kuchukua hatua stahiki ikiwemo kusitisha huduma za umeme pamoja na kuchukua hatua Kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wateja wenye tabia ya kuchezea mita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...